Alimpa namba yangu ya simu aje anisalimie sasa amenuna

markbusega

JF-Expert Member
Oct 12, 2015
826
847
Wasalaam wanajf

Mchumba wangu kipenzi ananishangaza sijajua hata nimueleweje!
Iko hivi mchumba wangu anarafiki yake ambaye yeye na rafiki yake niliwafahamu wote wakiwa pamoja wakati tukifanya kazi kwenye taasisi moja hapa nchini.

Mwanzoni nilivutiwa na huyo rafiki yake nikamtongoza hata yeye alifahamu kwa sababu wakati matongoza alikuwepo na alikuwa anasikia sikuona shida kwa sababu jinsi walivyokuwa marafiki wasingeweza kufichana kitu kujua hilo haikunipa shida. wakati tukidate nikaamua kughairi.

Baadaye niliamua kuhamia kwa rafiki yake ambaye ni mchumba wangu kipenzi.

Mchumba wangu alilia sana wakati namtongoza akawa ananifukuza kama mbwa ila nikakomaa naye hadi kikaeleweka

Baadaye tuliachana wote 3 tukaenda kusoma vyuo tofouti huko chuoni rafiki yake alipata mchumba wakaoana na wanawatoto wawili

Niliamua kukata mawasiliano na huyo rafiki yake sababu sikuona heshima kuwasiliana na mke wa mtu wakati mmewe hanifahamu ila mkewe (rafiki wa mchumba wangu) aliendelea kuhimiza tuwasiliane mara kwa mara nilipomueleza sio vizuri mke wa mtu mmeo kusikia unaongea na mwanaume ambaye hanifahamu, mara nyingi alijibu mmewe ni mpole hana shida hata mchumba wangu nilipomshirikisha hilo akasema wewe mpigie tu.

Sikuona umuhimu wa mimi kufanya hivyo na namba yake niliifuta

Kinachonifanya niandike post hii ni juzi rafiki wa mchumba wangu alipopata safari ya kikazi huku mkoani ninakoishi kwa vile anafahamu manispaa nilipo, aliomba namba yangu kwa rafiki yake (mchumba wangu)

Akampa na akaniomba nimpokee rafiki yake mgeni hajawahi kufika mji huo.

Kinachonishangaza sasa rafiki yake ambaye namwita shemeji anapopata mapumziko na wikend kama leo amekuwa akinitembelea na kurudi kituoni wanapofanyia kazi, mimi na mchumba wangu tuko mikoa tofauti, kila anaponitembelea mara zote akifika humpigia simu rafiki yake, kwamba yuko kwangu ili kuthibitisha hilo amekuwa akinipa simu yake naongea naye, nimekuwa najiuliza kwa nn anafanya hivi bila majibu.

Sasa jana wakati namsindikiza shemeji kumbe amepiga simu yangu mara 10 bila mimi kusikia kutokana na kelele za mziki uliokuwa unapigwa kwenye gari, nimejaribu kumpigia simu hapokei nimemweleza kwa sms haielewi
Kwa kweli mimi najiona sina kosa maana ninapojaribu kupunguza mazoea yeye ndiye amekuwa akituunganisha nipeni ushauri samahani kwa kuwachosha na uzi mrefu nawasilisha.






.
 
Back
Top Bottom