Alilaumiwa Magufuli kwa mambo ambayo ni ajenda ya chama

Dkt Mwijuma

Senior Member
Apr 9, 2023
198
561
CCM ni chama ambacho hakitaki uhuru wa habari miaka na miaka, Ni Nape Nauye ndiye aliezuia Bunge kuruka mbashara akiwa waziri wa habari, kipindi cha kampeni za uchaguzi mkuu 2015 na 2020 mikutano ya vyama pinzani ilikuwa hairuki live na hata kwenye taarifa za habari za media karibu zote habari za upinzani zilikuwa zinapewa mda kidogo sana na walichagua sehemu ya kawaida ndio inaenda live

Nadhani tunaona sakata la bandari hakuna media hata moja umerusha press ya mtu au watu wanaopinga mkataba achana na kurusha tukio live bali hata kuzionesha kwenye vipindi vyao vya taarifa za habari

Lkn tunaona CCM mda huu wapo mikoani na ziala za mikutano ya hadhara, juzi Kinana alikuwa Bariadi na akatoa lile tamko la bodaboda na trafic, lkn Chongolo pia yupo mzigoni vile vile, wote tunaona mikutano yao inaruka live lkn inaenda kwenye vipindi vya taarifa za habari karibia media zote nchini

Wakati huo huo CHADEMA nao jana wameanza mikutano hiyo, nimesitushwa sana kuona hakuna chombo cha habari hata kimoja kilichoonesha hata kwenye kipindi cha habari

Tulilalamika sana kuhusu watu kutekwa kwa JPM kina Ben Saanane, Azory nk tukasahau mambo kama hayo yalianza kitambo hichooo kina Dk Olimboka nk

Sasa hivi JPM hayupo tusidhani kesi za kupambikia zitaisha hivi ndio CCM ilivyo, hii ni ajenda ya chama
 
Back
Top Bottom