Usifanye mzaha na mambo ya kubakwa. Kubaka ni kitendo cha kinyama ambacho hakuna kitu mwanamke atafanya kifanye astahili kubakwa, hata kama ametembea uchi. Mwanaume anayebaka, au anaesifia kubaka ana matatizo ya akili na anahitaji msaada wa madaktari haraka.
Usije ukadhani hata siku moja kuna mwanamke duniani anaependa kubakwa, kwa sababu ikiwa mwanamke ana hamu ya ngono ni rahisi kumpata mwanaume wakati wowote. Hivyo kwa nini atake kubakwa ikiwa anaweza kupata mwanaume kirahisi tu? Wanaume ndio wasio na uwezo wa kupata mwanamke kila wanapohitaji - eidha watakataliwa, au watabembeleza sana, au kama wana hela watatafuta changu doa. Mwanamke hahitaji bidii kiasi hicho kupata mwanaume - hivyo hahitaji kubakwa.
umetoa ushauri mpk nimesisimka,chukua like mkuu.