Joshua Mulundi, aliyedaiwa kumteka Dr. Ulimboka akana mashtaka Kisutu

Huu ni uwongo wala hakuna haja ya kupoteza pesa na mawazo yetu kujadili uongo uliotungwa na TISS kwa kushirikiana na Kova na washirika wake. Kama alikodiwa basi ni Al Shaabab maana waliosema wataandamana kupinga maandamano ya madaktari tumewaona na kwa nini wanatataka kuandamana wanajua kwa sababu Dr. Uli alisema zaidi kwa madaktari wenziwe sasa mashaka na wasiwasi ni kama wakiamua kufanya kama ya Mwembe Yanga... itakuwa zaidi ya noma!!! Ndo bongo yetu tujipange waongo wasirudi 2015 mi nadhani ndilo suluhisho. Madaktari turudi tuchape kazi tukijua saa ya ukombozi inakuja, kila aliye na uwezo wa kuandika aelimishe jamii juu ya umuhimu wa mageuzi na 2015 watakuwa wao na gangsters wao wa Kenya kazi itakamilika kabla ya Nov.2015 kisha kama wakenya wataendelea kuwa chanzo cha kuleta ma-gangster tutafanya ya Charles Njonjo 1977 kuvunja EAC
 
Yaani Mkenya aje kumteka na kumhoji kiongozi wa madaktari Tanzania tena akitaka kujua ni nani wako behind mgomo..sipati picha huyu ganster alikereka vipi na mgomo wa madaktari..Kova ni noma!!
 
Siku zote za uhalifu asitubu aje atubu leo?
Tukio lenyewe linavyovuta hisia za watu halafu
eti wamempeleka kwa siri mahakamani.
Hivi kova haoni aibu kudanganya?Mbona mpango
wao huu ulishawekwa wazi hapa Jf?Hawakuwa na
mbinu mbadala?

there was no plan B.
 
[h=3][/h] [h=3][/h]


RAIA wa Kenya, Joshua Mulundi amepandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashitaka ya kumteka na kutaka kumuua Mwenyekiti wa Jumuia ya Madaktari Dk. Stephen Ulimboka.
Mulundi (21), ambaye ni mpishi mkuu alifikishwa mahakamani hapo jana saa 9 alasiri na kusomewa mashitaka mbele ya Hakimu Agnes Mchome.
Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya alidai kuwa Mulundi ambaye makazi yake Murang'a nchini Kenya anatuhumiwa Juni 26 mwaka huu, akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk. Ulimboka.
Katika shitaka la pili Mulundi anadaiwa Juni 26 mwaka huu, akiwa katika eneo la Msitu wa Mwabepande Tegeta, Dar es Salaam kinyume na sheria alijaribu kumsababishia kifo Dk. Ulimboka.





KWA HABARI KAMILI BOFYA HAPA
GUMZO LA JIJI: Kortini kwa kudaiwa kumjeruhi Dk. Ulimboka

 
Hii ni nukuu ya gazeti la Mwananchi la leo 15 July 2012Mkenya kukamatwaJoshua Mulundi, ambaye anatuhumiwa kumteka na kumtesa Dk Ulimboka alikamatwa na kupandishwa kizimbani katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam juzi alasiri na kusomewa mashtaka mawili na Wakili wa Serikali, Ladslaus Komanya.Wakili Komanya alidai mahakamani hapo kuwa, Mulundi ambaye makazi yake ni Murang'a nchini Kenya mnamo Juni 26, mwaka huu akiwa eneo la Leaders Club alimteka Dk Ulimboka.Hata hivyo, kumetokea utata wa jina, umri wake na makazi ya mtuhumiwa huyo.Wakati hati ya mashtaka mahakamani inasema ni Joshua Mulundi mwenye umri wa miaka 21, mkazi wa Murang’a nchini Kenya, taarifa ya Jeshi la Polisi imesema anaitwa Joshua Mahindi mwenye miaka 31 na mkazi wa Namanga nchini Kenya.Katika shtaka la pili, Wakili Komanya alidai kuwa tarehe hiyohiyo mshtakiwa alifanya jaribio la kumsababishia kifo Dk Ulimboka kwa kumpiga katika eneo la Msitu wa Pande eneo la Tegeta jijini Dar es Salaam, kinyume cha sheria.Hata hivyo, mshtakiwa huyo alikana mashtaka hayo akidai kuwa makosa aliyoshtakiwa nayo siyo sahihi. Hakimu Mkazi, Agnes Mchome alimwambia kuwa hatakiwi kujibu chochote kwa kuwa mahakama hiyo haina mamlaka ya kusikiliza shauri hilo, isipokuwa Mahakama Kuu pekee"
 
Hv kova hafahamu hilo kosa alilomshtaki nalo haliwez kusikilizwa ktk mahakama isiyo kuu? kabla ya yote kova atueleze
i) walisahau, walikosea aua walikuwa hawajua mahakama husika anayostahili kushtakiwa?
ii) why majina na umri vitofautiane?
iii) aje aeleze kwann anasema mengine na mchungaji anasema mengine?
 
If you want to cheat you be SMART enough. Know the rules first if you want to be a good player
 
Kama mshitakiwa alienda kanisani kutubu kwa jinsi tulivyojuzwa, sasa kwanini akane mashitaka. Hii ni ajabu na kweli!
 
Back
Top Bottom