Tungefanya majadiliano lakn anayepaswa kusimamia hayo majadiliano yaani serikali haamaniki kwa kila upande. Mi nafikir tukubaliane kutokukubaliana. Tubadilishane madaraka kwa misingi ya dini kama Lebanon. Wafanyakazi wasekta ya umma wawe wanaajiliwa na jopo la umoja wa kidini. Rais aachiwe kuteua mawaziri wake tu.
kwa waislam hakuna shida. vipi kwa wakristo munawalisha watu kibudu huko mitaani kwenu? maana mmeamua kuchija wenyewe.Mbona huku mitaani hakuna udini wowote?Twasoma tu kwenye magazeti na mitandao kama kuna udini.Huku twashirikiana na kuelewana vizuri,wapo waislam wameajiriwa na wakristo na wapo wakristo wameajiriwa na waislam na wengine ni dada wakazi,wanapewa heshima zote na kufanya ibada zao bila kuingiliwa na waajiri wao wa dini nyingine.
Muasisi wa udini tanzania ni ujinga!!!!
mjinga hujishuku, akijishuku hushuku
akishashuku, huhukumu tena kibudu
UJINGA NDIO MUASISI WA UDINI... ni duniani kote wala sio Tanzania tu, na udini ni ishara kubwa kwamba nchi husika ina wwajinga wengi
Unaikataa BAKWATA halafu unapongeza uamuzi wa kukutana Kadinali Pengo na Shekhe wa Dar Es Salaam ambaye ni wa BAKWATA!!!!!
Muasisi wa udini tanzania ni ujinga!!!!
mjinga hujishuku, akijishuku hushuku
akishashuku, huhukumu tena kibudu
UJINGA NDIO MUASISI WA UDINI... ni duniani kote wala sio Tanzania tu, na udini ni ishara kubwa kwamba nchi husika ina wwajinga wengi
kwa waislam hakuna shida. vipi kwa wakristo munawalisha watu kibudu huko mitaani kwenu? maana mmeamua kuchija wenyewe.
mkuu wala usibishe, kama unazungumzia kipindi cha uswazi basi uswahilini lina maana ya jamii duni kimaisha kama akina zambela wavyotuonyesha kwenye eatv kama ulivyotaja maeneo kama chang'ombe-dodoma. lakini kwa taarifa yako, mimi nimesikia haya maneno kwa masikio yangu mawili kutoka kwa wakristo wakimaanisha waswahili ni waislam. tena wakiona hata mtu kavaa kanzu au hijabu au kibarakashia tu. utasikia wakristo wanamuita mswahili. wala usibishe, mbona hayo maneno tunaishi nayo huku mitaani na dharau zenu hizo?
Ndugu KAUMZA unafikri walioanzisha neno Uswahilini ni watu wa Dinii gani? Halafu nikueleze kitu, neno
Uswahilini limeanzia huku Mikoa ya Pwani likasambaa mpaka Mikoani. Na leo Uswahilini inaweza kuwa Chang'ombe
Dodoma, Mabatini Mwanza nk...........
ungeacha hiyo nyekundu ya mwanzo tu maana ya mwisho sio applicable. anyway sina muda wakutosha kujibu thread yako. bye.Hapa sasa wewe ndo unaleta udini,kwa hivo mimi niliye mkristo naruhusiwa tu kufuga mifugo yangu lakini kuchinja sio kazi yangu...right?mwenye haki ya kuchinja ni wewe sio?na kiti moto utachinja?
Hebu tusilumbane hapa kwa ubinafsi wetu,au nikuulize swali,kwa nini sio kibudu kwangu mie mkristo ukichinja wewe Muislamu?wajua iman yangu wewe?
Ndugu ndio maana kuna nembo ya neno Halal food kwenye nyama zote alizochinja muislamu,maana yake zipo pia ambazo hajachinja muislamu!
Kwa hivo tusilazimishane kuchinjiana,chinja wako ntachinja wangu,nikipenda kula wako ni mimi,ukipenda kula wangu ni wewe,mambo ya kusakamana huyu kibudu na maneno mengine ndo yanazid kustawisha udini!
Bora uinywe ya mwisho mwisho, maana udini ukitawala hata hiyo bia hutaionja.
Mkuu ongeza font....macho ya uzee haya !!
Mbona yeye Abood Jumbe ndio alibobea kwenye suala la udini? Hadithi ya mwamba ngozi avutia kwake inatuhusu.Nyerere.
udini uliasisiwa na wakoloni,wakawarithisha watawala wazalendo...wazalendo wakaushikia bango bila kujua wamepandikiziwa mbegu mbaya watakayoivuna na kuila baadae,siku zikapita yakazuka ya kibiti,wabeba beramu za udini macho yakawatoka,huenda wanaamini yameisha na pengine hawatajirekebisha,mungu jaalia yawe yameisha...na kama bado basi wajaze hekima wabeba beramu wa udini wajali nchi yao zaidi kuliko imani zao ambazo hata hawazifuati ipasavyoTanzania hakuna udini ila watu wachache wanataka kutuaminisha hivyo kwa ajili ya maslahi yao binafsi
Sina uhakika sana km lengo la dini lilikua kugawa watu! Maana leo tukiwa kwenye say michezo huwezi kujua ni yupi Mkristu,ni yupi Muisilamu na ni nani asiye na dini lakini tukirudi mtaani wakati wa kuabudu ndipo utaona mgawanyiko!
Ilikua Alhamis,siku moja kabla ya siku ya Pasaka(Ijumaa kuu)kwa masikio yangu namsikia Imamu mmoja wa msikiti mmoja wa jirani na mahali ninaishi akiwataka wazazi ambao ni Waisilamu wasiwaandae watoto wao kusherehekea sikukuu ya pasaka kwani kufanya hivyo ni kwenda kinyume na mafundisho ya Mtume..nimekaa chini na kutafakari sana kwamba hatujafikia hapo..
Leo tutaanza na hili la kuwatenga watoto,kesho jirani wa chumba cha pili atakuitia chakula(kwa tunaoishi kwenye nyumba za kupanga) utakataa kwa kua ni wa dini tofauti,keshokutwa utaumwa utamgongea jirani hatofungua mlango kwa kua hamuaminiani kuanzia kwenye chakula na mengine na mengine...mwisho wa haya yote ni nini?
JF tunahitaji great thinker kama hawa! Wenye mitazamo ya udini ni wajinga tuu, mojawapo ya mihadarati (opium) ya hizi dini hizi ndio udini wenyewe