Habibu B. Anga
JF-Expert Member
- May 7, 2013
- 6,557
- 25,716
Juzi nilitamani nimtafute Ali na kumpongeza personally kwa kuwataka watu wampigie kura Dee sababu niliona sasa angalau wasanii wetu wameanza kukomaa na kuacha mambo ya kitoto! Ni kitu kizuri na cha kusifika..
Lakini baadhi ya watu wamepata ukakasi kidogo (mimi nikiwemo)! Binafsi situmii sana mtandao wa instagram huwa nahudhuria huko pale kunapokuwa na 'big news' huko instagram.. Jana baada ya kuhudhuria huko nikashangazwa na maajabu niliyoyakuta huko, maajabu ya karne!! Kuna watu wameanzisha kampeni ya kuhamasisha watu wasimpigie kura Diamond Platnumz na apigiwe kura msanii Wizkid au Yemi Alade.. Na watu hawa wanaohamasisha ni watu wa karibu kabisa na Ali pamoja na Mlimbwende wetu Sepetu! Ni watu ambao ingawa wanatumia username "fake" lakini wanafahamika kabisa na masters wao..
Binafsi namuona Ali kama mtu asiye na makuu na mtu mnyenyekevu, kwahiyo napenda kuamini kuwa alimaanisha pale aliposema watu wampigie kura Diamond, kinachonishangaza ni kwanini anaruhusu hizi zinazoitwa "team" zake kufanya uhamasishaji wa kipuuzi dhidi ya mtanzania mwenzao! Ni kwanini swahiba wake Sepetu anaruhusu watu wake wafanye uhamasishaji huo.. Hizi timu hazipindui kwa Ali au Sepetu, yeyote kati yao akiweka post moja tu ya kuwakanya wote wanafyata mkia, nawaza kwanini Ali anashindwa kujiweka mbali na huu upuuzi.. Nirudie, viongozu wa hizi timu wanafahamiana personally na kina Sepetu na Ali!!
Tusisahau kuwa Dee ni binadamu na hajatolewa nyongo, kinapofanyika kitu kama hiki anaona! Kwahiyo pale anapoamua kujiweka mbali na baadhi ya watu, wengine wanadhani ana ringa lakini ukweli ni kuwa anafahamu kuna watu wanamuombea dua za kishetani kutwa kucha!
Nina imani kabisa Dee ataendelea kuipeperusha vyema bendera ya nchi yetu na kuwaabisha wanaokesha kuomba dua za mashetani!! Pia natamani kuona Ali akijiweka mbali na hizi kampeni za kipuuzi kulinda heshima yake na kile alichokisema EA radio kiwe na maana..
Yote kwa yote nakupongeza kwa ile kauli, na ni mwanzo mzuri kwa sisi tunaotamani huu utoto uishe!!