Singida ndio home
JF-Expert Member
- Feb 23, 2012
- 3,188
- 3,367
Ukiuzungumzia mziki natural basi ni ule mziki ambao ni mzuri masikioni. Siku hizi ni wachache sana wanaoweza kutoa nyimbo bila video na bado zikapendwa. Miongoni mwa hawa wachache basi Ali Kiba hakosi.
Kuna msemo ule "Mwanamziki akizima ndio kwaheri" Ali kiba aliupindua baada ya kukaa kimya muda mrefu kwa hiari yake na kurudi kwa spidi isiyo na kifani wa ngoma kama za Mwana na Chekecha.
Ngoma nyingi bila video hazibambi mfano ni majuzi nilidownload audio ya shetta "Namjua", kiukweli sikuvutiwa nayo ila baada ya kuiona video yake ndio walau nilianza kuipenda. Pongezi ziende kwa director wa video.
Ila cha kushangaza majuzi juzi tu ngoma ya Ali Kiba nilidownload audio bila kuiona video yaani aisee ngoma ni tamu mno. Jamaa kuanzia ngoma zake cinderella, hadithi, far away, usiniseme, run dunia , mac mugga, nakshi nakshi, dushelelem, nichum, mwana, chekecha, nagharamia khaaa tutakesha hapa nyimbo zake zinaeleweka bila hata video.
Nisiwe mnafki kiukweli mimi ni mshabiki dam dam wa Diamond ila Diamond nachomkubaliaga sana ni mjanja sana yupo sharp hata akiwa stejini anachangamsha, ni msanii mwenye nyota ya kupendwa na kupata pesa na umaarufu tofauti na Ali Kiba ambae mziki wake umebase sana kwenye kuimba tu.