Algeria: Mamia waandamana kupinga Rais Abdelaziz Bouteflika kugombea tena Urais

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,877
6,326
Waandamanaji hao wameandamana kwa siku ya pili mfululizo hapo jana katika mji mkuu, Algiers wakimpinga Rais wa sasa Abdelaziz Bouteflika kugombea tena urais kwa awamu ya tano

Waandamani hao ambao idadi yao ya jana ilionekana kupungua kulinganishwa na ile ya juzi Ijumaa wamesema hakutakuwa na awamu ya tano kwa Rais huyo kwani hawataki ashiriki uchaguzi Mkuu utakaofanyika Aprili 18, 2019

Bouteflika ambaye anaongoza nchi hiyo tangu mwaka 1999, hivi karibuni ameonekana kwa nadra hadharani tangu augue kiarusi mwaka 2013 na kwa mujibu wa ofisi yake atasafiri leo kwenda Switzerland kwa matibabu

Tangu achaguliwe na chama tawala cha FLN kugombea tena, vyama kadhaa vya kisiasa na Mashirika ya biashara yameshasema hayatamuunga mkono japokuwa anatarajiwa kushinda kirahisi kutokana na Upinzani kuwa dhaifu na uliogawanyika

IMG_20190224_022510.jpg


====

Hundreds of Algerians protested for a second straight day on Saturday in the capital against President Abdelaziz Bouteflika's plan to seek a fifth term.

The turnout was smaller than on Friday when thousands took to the streets of Algiers and other cities against the 81-year-old leader's decision to stand in the April 18 presidential election.

Bouteflika, in office since 1999, has been seen in public only a handful of times since suffering a stroke in 2013.

"There won't be a fifth term," said Said Kamel, who took part in the protest in central Algiers.

Bouteflika will travel on Sunday to Switzerland for medical checks, his office said on Thursday, without giving details.

The ruling FLN party has picked him as its presidential candidate. Several political parties, trade unions and business organizations have already said they would back him, and he is expected to win easily as the opposition remains weak and divided.

Strikes and protests over social and economic grievances are frequent in Algeria, but are generally localized and do not touch on national politics.

More than a quarter of Algerians under 30 are unemployed, according to official figures, and many feel disconnected from a ruling elite made up of veteran fighters from Algeria's 1954-1962 independence war with France.

Bouteflika remains popular with many Algerians, who credit him with ending a long civil war by offering an amnesty to former Islamist militant fighters.



Sent using Jamii Forums mobile app
 
Kwakweli wanadamu hapo kwenye tamaa pamesha tushinda kabisaa sasa mtu katawala tokea 1999, na anakiharusi sijui ndio kupooza?lakini bado anatamaa ya kuendelea kukikalia kiti hicho, kwanini lakini tamaa yakuto kutosheka inatusumbuwa sana wanadamu?kasahau nini kuwafanyia wananchi ndio anataka kuwa fanyia sasahivi?kwani bila yy hiyo nchi Algeria haitasonga?Mungu atunusuru kwa hii tamaa ya vya ulimwengu huu.
 
Naendelea kuogopa wasimwambukize hata rais wetu naona hata algeria ,Rais wake anataka kujiongezea Muda,

Kumbuka Mseven kaongeza, na Bashir naye kaongeza ,dha

 
Napata feelings kuwa Brit mzee wa Urusi ni mbunge mstaafu mwenye mixed feelings, ya kwanza anaichukia CCM kwa kuwa wameshindwa kumpatia jimbo lake la muda mrefu lakini pia anaipenda CCM kwa kuwa imekuwa maisha yake kwa muda mrefu.
mods msinipige ban sijamtaja member yoyote wa humu JF
 
Napata feelings kuwa Brit mzee wa Urusi ni mbunge mstaafu mwenye mixed feelings, ya kwanza anaichukia CCM kwa kuwa wameshindwa kumpatia jimbo lake la muda mrefu lakini pia anaipenda CCM kwa kuwa imekuwa maisha yake kwa muda mrefu.
mods msinipige ban sijamtaja member yoyote wa humu JF
Mkuu siyo hivo wala si jimbo ishu ni kuogopa yaendeleayo
 
Bouteflika amekaa ikulu kwa takriban miongo miwili hivyo haamini kama kuna maisha nje ya ikulu. Keshakuwa kama samaki majini. Very hopeless indeed.
 
Wenzao Uganda kupitia Vuguvugu la MRA Cha Rais Museven wamepitisha jina La Rais Museven Kuwa Mgombea Urais wa Uganda kwa Miaka 50 bila ya kupingwa

Yaan kuanzia 2021-2071 Chama hicho kimempitisha Museven Kuwa Mgombea Urais bila ya kupingwa wakati Sasa hivi Museven ana Miaka 75!

Africa kuna virutubisho vya akili tumekosa bila shaka
 
Back
Top Bottom