Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 4,393
- 14,500
Viongozi wa dini mbalimbali nchini wanatarajiwa kufanya Tamasha kubwa la Maombi ya kuombea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwaka huu.
Akizungumza na vyombo vya habari Mkurugenzi wa Msama Promotions, Alex Msama ambao ndio waandaaji wa tamasha hilo amesema tamasha litafanyika tarehe 21 mwezi wa sita na litafanyika kwa mikoa 26 nchini.
"Ni tamasha kubwa sana lakini lengo kubwa la tamasha hili ni kuombea uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika katika nchi yetu mwaka huu" amesema Msama
Msama ameeleza kuwa baada ya Dar Es Salaam tamasha hilo litaendelea katika mikoa mingine ambapo ameeleza kuwa wanatarajia kufanyia uwanja wa Benjamin Mkapa au uwanja wa Uhuru endapo watapata kibali.
Kupata matukio na taarifa zote kwa kila mkoa kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025 ingia hapa: Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025
Aidha ameeleza kuwa pamoja na watumishi na viongozi wa dini waimbaji mbalimbali kutoka ndani na nje ya nchi kama Rwanda, Nigeria na Afrika Kusini wameshazungumza nao huku wale wa nyumbani wakisuibiri tu tarehe kufika waweze kushiriki.
Kwa upande wake Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la FPCT Philipo Mdaraga amesema maombi yana umuhimu mkubwa kwa uchaguzi ili kutoa nafasi kwa Mungu kusaidia ufanyike kwa amani na utulivu pia kupaya viongozi wanaosyahili.
Naye Mchungaji Rose David wa Kanisa la Saa ya Ukombozi ni Sasa pia amesisitiza ushirikiano wa viongozi wa dini na watanzania kujitokeza kushiriki katika maombi hayo.