Alert!!!!!!!Desemba ni mwezi wa mavuno mpaka mwaka mpya upite!

kilimasera

JF-Expert Member
Dec 2, 2009
3,068
270
Kwa mnaosafiri iwe kwa mabasi au usafiri binafsi muwe makini sana barabarani hasa kwa kipindi hiki cha mwisho wa mwaka na mwaka mpya kwa kuwa kihistoria kila mwaka inapofikia wakati kama huu ajali zinakuwa nyingi sana kupita kawaida hasa za mabasi na magari binafsi!na ndicho kipindi ambacho watu wanasafiri sana kwenda makwao kusheherekea skukuu na familia zao kwa hiyo kuweni makini na mkiona dereva anakimbia bora mkamwambia kabisa apunguze mwendo ingawa huwa ni ngumu sana kwa abiria kuwaambia madereva neno hilo kwani wengi hupenda kuwahi kufika kumbe matokeo yake huwa ni kuwahi kufika kwa mungu!familia nyingi yaani baba,mama na watoto huteketea sana kwa kipindi hiki kutokana na ajali hivyo sishauri sana watu kusafiri katika makundi kwa kutumia usafiri binafsi vinginevyo muwe waangalifu sana!!!nimeandika hivi baada ya kusikia kwamba tayari mavuno yameshaanza na leo basi la super feo limedondoka katikati ya songea na njombe!
 
Na hao madereva wanavyokimbizaga mabasi utadhani wao hawaogopi kufa!Inabidi abiria waamue wenyewe...kuchelewa makwao au kuwahi mbinguni!
 
Back
Top Bottom