Zamani tulikuwa tunatunza picha zetu kwenye album na pindi mgeni akija unampa anaangalia sasa hivi Facebook kama ndo album ya kisasa watu wanayotunzia picha zao h
Alikuwa akija mgeni anapewa album ya picha anaangalia, mnacheka na kufurahia maisha. Siku hizi mgeni akija utasikia "mna chaja ya smatifoni?, naomba mnisaidie maana simu yangu karibia inazima."
Alikuwa akija mgeni anapewa album ya picha anaangalia, mnacheka na kufurahia maisha. Siku hizi mgeni akija utasikia "mna chaja ya smatifoni?, naomba mnisaidie maana simu yangu karibia inazima."
Sisi ndugu wote tunachekiana kwenye group la ukoo(whatsapp)
hakuna kutembelea hadi kuwe kuna tukio muhimu,ubatizo,vipaimara,harusi,kuzaliwa mtoto,msiba au ugonjwa tu...
Kweli aiseee....nakumbuka enzi hizo tulikuwa tunafunga safari kwa mguu kwenda kwa bibi, tunapita vijiji viwili tukiwa tumebeba na zawadi kama nafaka na mboga. Tukifika huko tunakaa kama wiki, wakati wa kurudi nao wanatusindikiza mpaka nyumbani. Nao wanakaa wiki kisha wanarudi kwao.
Siku hizo, siku hizi pamoja na kuboreshwa kwa miundombinu ya usafirishaji kila mtu anazunguka kwenye malango yake tu.