Alasiri ya Ijumaa: usikose!

Slim5

JF-Expert Member
Jan 7, 2014
25,522
2,000
kwa wale wenzangu na mimi, fanya chochote kati ya haya Ijumaa ya keshokutwa, ila usithubutu kuangalia "Tv zao"
 1. Ijumaa Alasir mazoezi ya Yanga, yataendelea pale uwanja wa LOYOLA, Mabibo!
 2. Ijumaa Alasir mazoezi ya Simba, yatakuwa UWANJA WA BOKO VETERAN!
 3. Ijumaa Alasir msikose kuja kuangalia kombe la Mbuzi, Uwanja wa Makurumla!
 4. Ijumaa Alasir Kinesi kama kawa, kuna game tamu sana!
 5. Ijumaa Alasir mazoezi kama kawaida pale Vingunguti uwanja wa Fc Cologne kwa kina Shaban Kisiga "Marlone"
 6. Ijumaa Alasir LEADERS hakutakuwa na Twanga
 7. Ijumaa Alasir naomba mje hapa, ntakuwa nasimulia bonge la love story
 8. Ijumaa Alasiri hatutakata umeme, ndio siku nzuri ya kuongezea idadi ya siku za extra duty
 9. Ijumaa Alasir tembelea Sewa Haji, Kibasila, Mwaisela, Amana, Temeke yaani Hosp yoyote ya jirani na wewe!
 10. Ijumaa Alasir kuna kipindi cha taarabu, nimesahau channel, nitawaambia baadae!
 11. Ijumaa Alasir chukua familia yako mkawatembelee wale mliowamiss!
 12. Ijumaa Alasir piga zako usingizi!
 

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,490
2,000
Mweeeh..! Atakaekuwa ameelewa hii naomba anisaidie na mie..:A S-confused1:
 

sosoliso

JF-Expert Member
May 6, 2009
8,490
2,000
Ili mradi tu usiisikilize hotuba ya msanii maarufu hapa nchini le profeser jk na wazee wa ccm dsm
Ha ha ha ha lol.. Ahsante sana maana Mwana JF ameipiga kifasihi.. Mie nitakuwa kwa ofic na sitoki mpaka saa 4 usiku..
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom