Alama ya mgogoro mzito ndani ya mabaki ya CCJ (CCK)

Alama ya mgogoro mzito ndani ya mabaki ya CCJ (CCK)

silaha

Member
Joined
Jun 8, 2012
Posts
60
Reaction score
34
Tamko la kupinga Chama Cha Kijamii (CCK) kushiriki Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25 Oktoba, 2015​
Chama Cha Kijamii (CCK) kimekosa sifa za kushiriki kwenye Uchaguzi Mkuu wa tarehe 25/10/2015 kwa sababu zifuatazo:
1. Kuna kesi mbili Mahakama Kuu Dar Es Salaam dhidi ya viongozi wa Chama (CCK).

(i) Kesi ya msingi inayomtuhumu Bwana Constantine Akitanda kuitisha Mkutano Mkuu wa uchaguzi wa ndani wa Chama kinyume na katiba ya CCK wala kupitia utaratibu unaokubalika kwa kugushi wajumbe wa Mkutano Mkuu wa tarehe 19-4-2015. Uchaguzi huo ulizuiwa kwa amri ya mahakama, ambapo wakati zuio hilo linapokelewa na wahusika, mwenyekiti, makamu wenyeviti na wajumbe wa Kamati Kuu wa kuchaguliwa walikwishajiuzuru. Na kwa kuwa hakuna uchaguzi mwingine uliofanyika hadi sasa, watu hao waliojiuzuru wanabaki kuwa si viongozi wala si wajumbe tena wa Kamati Kuu.Na hivyo kufanya wajumbe wa Kamati Kuu waliobakia, ambao si wakuchaguliwa kwenye Mkutano Mkuu (wakiwemo katibu mkuu na watendaji wake), hawatoshelezi kuunda Kamati Kuu halali. Kukosekana uhalali wa Kamati Kuu, kunafanya shughuli za Chama kukwama, ikiwa pamoja na kuwajadili na kuwateua wagombea wa nafasi za ubunge, na kupendekeza wagombea wa nafasi za urais kwenye Mkutano Mkuu.

(ii) Kesi ya Kudharau Mahakama.
Kesi hiyo inawahusu viongozi wakuu watano: Mwenyekiti, Makamu Wenyeviti (2), Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, na Mwenyekiti wa Kitengo cha Wanawake. Hao wanatuhumiwa kuendelea na uchaguzi hata baada ya kupata zuio la Mahakama Kuu, na hivyo kupelekea tuhuma ya kuidharau mahakama.

2. Chama Cha Kijamii hakina wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa, kwa sababu Chama kimeshindwa kufanya uchaguzi kuwapata wajumbe hao. Kwa hiyo, hata kama taratibu zingine zingekuwa sahihi, haiwezekani wagombea urais kuteuliwa na kupitishwa kutokana na kikao hicho hakiwezi kuitishwa kwa mujibu wa Katiba ya Chama.

3. Chama Cha Kijamii hakina viongozi katika ngazi zifuatazo: Shina, Tawi, Kata/Shehia wala Jimbo. Chama kimeshindwa kuhamasisha na kusimamia uchaguzi katika ngazi hizo. Kukosekana uongozi halali wa Chama kwenye ngazi hizo, kunafanya Chama kisiweze kutekeleza majukumu yake, hasa ya kawateua wagombea katika ngazi husika. Na hivyo kukosa uhalali wa kushiriki Uchaguzi Mkuu.

4. Chama Cha Kijamii hakina Bodi ya Wadhamini. Hakuna uchaguzi uliofanyika. Kwa kukosa Bodi ya Wadhamini, ni kukiuka sheria ya Vyama vya Siasa, na hivyo kukosa sifa ya chama halali.
5. Chama Cha Kijamii kimekosa sifa ya kutambulika kisheria kama chama cha siasa, kwa sababu kimeshindwa kufanya chaguzi zake za ndani ili kupata viongozi wa kudumu. Kinachofanya chama hicho kiendelee kuwepo, ni kesi zilizopo mahakamani, ambazo zinamfunga Msajili wa Vyama vya Siasa asikifute. Sheria ya vyama vya siasa inavitaka vyama cha siasa kufanya chaguzi za ndani katika muda usiozidi mwaka mmoja baada ya kupata usajili wa kudumu. CCK ilipata usajili wa kudumu tarehe 27Januari mwaka 2012 na hadi sasa kimeshindwa kukidhi matakwa ya sheria hiyo.

Kwa sababu hizo, Chama cha Kijamii hakina sifa za kushiriki Uchaguzi Mkuu.
Katika siku za hivi karibuni amejitokeza mtu kutaka kugombea nafasi ya urais kupitia Chama Cha Kijamii (CCK). Vyombo vya habari vimenukuliwa kuwa mgombea huyo, Mchungaji Dkt Gogfrey Malisa, ameshachukua fomu kutoka CCK. kunachoonekana ni kuwa, mgombea huyo mtarajiwa hana nafasi ya kupitishwa na kuteuliwa na Chama, kwa sababu Chama hakina uhalali wa kufanya hivyo, kama ilivyoelezwa hapo juu. Hivyo, mpango mzima wa kuendeleza mchakato huo wa kumpata mgombea urais na wagombea wengine, ni batili. Na iwapo wahusika wataendeleza harakati hizo, itakuwa ni udanganyifu na bila shaka itapelekea kuwekewa pingamizi mahakamani.
Zoezi hilo linafanywa bila kushirikisha Katibu Mkuu wetu halali, Bwana Kassim Mtalam, ambaye ni mtendaji mkuu wa Chama, kitendo ambacho kinaonesha kuwa mpango huo ni batili.




KATIBU MKUU WA CHAMA.
KASSIM MTAALAM.
11/07/2015
 
Wapenda mabadiliko na wanaotaka mabadiliko karibuni ACT WAZALENDO,huku hakuna ubabaishaji uliopo kwa akina mbowe,lipumba na akina mbatia,ukija huku kazi ni moja tu,kufyeka mapori.
 
Tatizo n nn haswa, kutomshirikisha katibu mkuu wa chama au kutotimiza masharti ya kanuni na taratibu.

Polymer wa azaboy
 
halafu tunathubutu kusema kuna upinzani wa dhati Tanzania. Go go ccm
 
Wapenda mabadiliko na wanaotaka mabadiliko karibuni ACT WAZALENDO,huku hakuna ubabaishaji uliopo kwa akina mbowe,lipumba na akina mbatia,ukija huku kazi ni moja tu,kufyeka mapori.

Vipi kwa akina kinana hakuna huo ubabaishaji?
 
Vipi kwa akina kinana hakuna huo ubabaishaji?

sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha akina nana,toka naanza siasa miaka 15 iliyopita niko katika vyama vya upinzani,so ubabaishaji wa wapinzani wenzetu naujua sana kuliko wa akina nana!
 
sijawahi kuwa mwanachama wa chama cha akina nana,toka naanza siasa miaka 15 iliyopita niko katika vyama vya upinzani,so ubabaishaji wa wapinzani wenzetu naujua sana kuliko wa akina nana!

sasa mkuu unafanya nini na hawa wababaishaji?.

huoni km nawe utakuwa mbabaishaji?.
 
Back
Top Bottom