AL-SHABAB YAUA WAWILI KENYA

AL-SHABAB YAUA WAWILI KENYA

Dalton Elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
970
Reaction score
1,978
Watu wawili wameuawa kwenye kijiji cha Taa kilichopo kaunti ya Lamu nchini Kenya kwenye siku ya sikukuu ya Krismasi.

Eneo hilo la Taa liko jirani na msitu wa Boni ambapo vikosi vya ulinzi vimekuwa vikifanya operesheni za kijeshi tangu mwaka 2015 kwa ajili ya kuviondoa vikundi vya wapiganaji wa msituni wakiwemo wapiganaji wa kundi la Al Shabaab.

Msitu huo ambao uko karibu ya mpaka wa Kenya na Somalia na maeneo ya karibu na msitu huo yamekuwa yakiriootiwa kuvamiwa na wapiganaji wa msituni mara kwa mara na kufanya mashambulizi kwa raia.

Jeshi la polisi nchini Kenya limesema washambuliaji hao walivamia vijiji vilivyopo maili kadhaa kutoka eneo la kitalii la Lamu na walilenga kuwashambulia wanachi kwa uratibu uliowekwa vizuri.

Wanakijiji walionusurika na mashambulizi hayo wamesema kuwa walikimbia na kujificha msituni wakati kundi la wapiganaji wa msituni lilipovamia na kuanza kufanya mashambulizi.

Kamishna wa polisi wa mkoa wa Pwani John Elungata amesema wanakijiji na wananchi wa Kenya kushirikiana na jeshi la polisi ili kukabiliana na wapiganaji hao.
SOURCES AZAM TV
 
Pole sana Kwa hao wanakijiji. Al shabab Sijui kwanini hupenda kuua watu wasio na hatia kwao.
 
Back
Top Bottom