Al-Shaabab wakiri kufanya shambulio na kudai wameua wanajeshi 57 wa Kenya

Kurzweil

JF-Expert Member
May 25, 2011
6,621
8,411
Kundi la Al-Shabab nchini Somalia limesema wapiganaji wake wameshambulia kambi ya wanajeshi wa Kenya wanaohudumu chini ya kikosi cha Umoja wa Afrika (Amisom)nchini Somalia.

Wapiganaji hao wanadai kuwaua wanajeshi wengi kwenye shambulio hilo katika kambi ya Kulbiyow kusini mwa Somalia karibu na mpaka wa nchi hiyo na Kenya.

"Mujahideen (wapiganaji) wawili walivurumisha magari yaliyokuwa na mabomu na kuyalipua kwenye lango la kambi hiyo ya mji wa Kulbiyow kabla ya wapiganaji wengine kuingia. Baada ya makabiliano makali, tumefanikiwa kuiteka kambi," mmoja wa wasemaji wa al-Shabab Sheikh Abdiasis Abu Musab ameambia shirika la habari la Reuters.

Msemaji huyo amedai kundi hilo limewaua wanajeshi zaidi ya 50 na kutwaa magari na silaha za wanajeshi hao, taarifa ambazo msemaji wa majeshi ya Kenya amekanusha.

Kanali Paul Njuguna ameambia Reuters: "Ni uongo. Operesheni ya kijeshi inaendelea. Tunaendelea kupokea taarifa."

Al-Shabab wamekuwa wakipigana dhidi ya serikali ya inayoungwa mkono na mataifa ya magharibi na jamii ya kimataifa.

_93833828_somalia_control_624_v2_swahili.png

Wanajeshi wa Kenya pamoja na wanajeshi kutoka Djibouti, Uganda na Ethiopia, chini ya Amisom, wamekuwa wakisaidia serikali hiyo yenye makao yake Mogadishu.

Januari mwaka uliopita, wapiganaji wa al-Shabab walishambulia kambi ya majeshi ya Kenya el-Adde na kuua wanajeshi wengi.

Al-Shabab walisema waliua zaidi ya wanajeshi 100. Jeshi la Kenya halijatangaza idadi kamili ya wanajeshi waliouawa hadi wa leo.

Chanzo: BBC/Swahili

======
UPDATE

Kundi la kigaidi la Al Shabab limekiri kufanya shambulio kwenye kambi ya jeshi la Kenya nchini Somalia leo asubuhi na kuwaua wanajeshi 57.

TAZAMA HABARI HII IKISOMWA KTK JAMIILEO
 
Kdf must learn the lesson and retreat swiftly, these militia men are stupids who don't care for anything, they commit mass killing through bomb suicides, Kenyans must agree that they have been working for nothing and in price of deaths and losses!!
Please Kenyans retreat, withdraw your men from the zone, otherwise all of them will be squashed and smashed as tomatoes,
 
NAIROBI, Kenya, Jan 27- Kenya Defence Forces Spokesman Lieutenant Colonel Paul Njuguna says KDF soldiers managed to repulse Al-Shabaab militants Friday morning following an attack at their camp in Kulbiyow town in Lower Jubba region of Somalia.

He said heavy fighting ensured between the militants and KDF soldiers but they managed to repulse the aggressors during the dawn attack.

Njuguna told Capital FM News that the soldiers who operate under AMISOM were clearing the area to ensure the threat was fully eliminated.

“We have killed a number of them but a comprehensive report is coming,” he assured.

“It is not true that the Al-Shabaab overrun our camp. It was an attempted attack which has been repulsed,” he clarified.

While he confirmed that several terrorists were killed, it is not yet clear whether the KDF suffered any casualties.

The attack comes a year after the El Adde incident in which a camp was overrun and more than 100 Kenyan soldiers killed.
 
wapo busy kujenga ukuta wa waya!!
hahaha Akili zingine bwana!!
RPG moja inafumua waya na kuacha njia
wanaume wanajipitia kiurahisi!!

Madaktari wamegoma wananchi wanajifia
wenyewe wanajipitishia mpango wa DILI!!


Alshabaab wapo Kenya
huo uzio nikupoteza muda tu
 
Hilo ni shambulio la woga... Poleni sana... Muongeze survaillabce na kuimarisha vizingiti hasa kwenye njia zinazoingia kwenye base zenu...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom