Al Ahly wametuzidi kila kitu, na wamekuja

Al Ahly wametuzidi kila kitu, na wamekuja

kbm

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2012
Posts
5,224
Reaction score
1,686
YANGA-VS-AL-AHLY.png


Mchezo wa hatua ya Pili wa Klabu Bingwa Afrika, kati ya Mabingwa wa Tanzania Bara, Yanga SC na Mabingwa wa Afrika, na Misri, Al Ahly, utafanyika jijini Dar es Salaam siku ya Jumamosi.




Wamisri. Wana uwezo mkubwa wa kutuhesabia jinsi walivyotuzidi kwa kila kitu. Uchumi, soka, mipango, historia. Na hata dhambi nazo wametuzidi. Historia yao ya mauaji ya kinyama siku za karibuni yanadhihirisha hilo.
Na hata wakati Al Ahly ya Misri ikijiandaa kucheza na Yanga katika pambano lake la raundi ya kwanza la Ligi ya Mabingwa Afrika, inaonekana kama vile wameizidi Yanga kila kitu. Kuanzia soka lao, uchumi wa klabu na hata dhambi.
Al Alhy wapo hapa jijini Dar es Salaam. Wamejikita katika kuichunguza Yanga. Hata hivyo asilimia 90 ya hali halisi ni kwamba wanapewa nafasi kubwa ya kuitupa Yanga nje ya mashindano. Lakini wameiheshimu Yanga.

Yanga hawajali sana. Wao wapo wapo tu. Furaha yao kubwa katika siku za karibuni ilikuwa ni kuwachapa Mbeya City. Baada ya hapo wakafurahia sare ya watani zao Simba na Mtibwa pale Uwanja wa Jamhuri, Morogoro.
Baada ya hapo wakafurahia ushindi wa mabao 7-0 dhidi ya vibonde Komorozine katika pambano ambalo wachezaji watatu wa Yanga wangeweza kucheza mechi wakiwa wamefumba macho na bado timu yao ingeshinda.

Baada ya hapo Yanga wamejikita katika kufurahia kichapo cha bao 1-0 ambacho watani zao wamepata kutoka kwa Mgambo. Lakini wakati Yanga wakifurahia kichapo cha Simba kwa Mgambo, kocha Msaidizi wa Al Ahly, Ahmed Ayoub na skauti mkuu wa timu hiyo walikuwa Uwanja wa Chamazi kuomba kutumia huduma za kisasa za uwanja huo wakati wa mechi yao dhidi ya Yanga.
Hapa ndipo unapogundua kuwa tunaishi katika dunia mbili tofauti. Mechi ya Yanga na Comoro ni wazi kuwa imeshamalizika. Lakini ni namna gani Yanga wanajiandaa kucheza na Al Alhy? Hauwezi kujua.

Kabla hata Yanga hawajaingiza timu kucheza na Comoro ilikuwa ni wazi kwamba Wacomoro walikuwa wamejifia. Walipaswa kuanza kuichunguza Al Ahly mapema zaidi. Walipaswa kujua timu yao itafikia hoteli gani Cairo, itafanyia mazoezi wapi, na hoteli yao iko umbali gani kutoka uwanjani.
Walipaswa kujua ni timu gani wanaweza kucheza nayo Afrika Kaskazini kabla ya kwenda Cairo.
Sijui kama wamejipanga kwa hili mapema, lakini kwa wenzetu mechi ya soka ina maandalizi ya muda mrefu. Kwa sisi Watanzania utakachoweza kusikia baada ya Yanga kuitoa rasmi Comoro ni kwamba ¡®Tunamtafutia kocha mikanda ya Al Ahly¡¯.

Hapo unakuta kocha anatafutiwa mikanda ya Al Ahly ya misimu mitatu nyuma. Unakuta baadhi ya wachezaji wamehama, kocha amebadilika, timu imeingiza wachezaji chipukizi. Na bado unajisifu kuwa umeisoma timu katika mkanda wa video.
Wao wamekuja kuitazama Yanga. Wameshajua kuwa Mrisho Ngassa na Simon Msuva wana kasi na walinzi wao watakabia mstari wa kwanza wa uwanja. Wanajua Frank Domayo ni injini ya timu na hapaswi kugeuka mara nyingi kuichezesha timu.

Hii ndio sayansi ya soka. Sisi tunaiangalia siku ya leo halafu basi. Hatuangalii sana mahitaji ya siku ya kesho. Ndiyo maana wenzetu, kama hawa Wamisri wametuzidi kila kitu. Hata dhambi!




Mspoti
 
Watanzania tukiwa na kumbukumbu mbaya ya timu zetu kushindwa kutamba mbele ya timu za Misri.
Ni timu ya Simba tu, walau inaweza kuwa na historia japo kwa uchache juu ya timu za kutoka Misri, walipokutana na mara chache iliweza kujivunia.
Mwaka 2003, Simba iliweza kuwaondosha Mabingwa wa nchi hiyo, timu ya Zamalek, baada ya kushinda bao 1-0 jijini Dar es Salaam, kabla ya kushinda 3-2 kwa njia ya penati katika Uwanja wa ugenini.
Ukiacha historia hiyo kwa Simba dhidi ya Zamalek, bado timu hiyo ina chakujivunia kwa timu ya Mafulira Wandarers ya Zambia, mwaka 1979 baada ya kuchapwa bao 4-0 kwenye uwanja wa Taifa, kabla ya kushinda bao 5-0 ugenini.
Ni ushindi mkubwa ambao bado unakumbukwa na wengi na ukishangaza pia. Nimejikuta nikianza hivi kwa kuangalia mechi ijayo ya Yanga dhidi ya timu ya Al Ahly ya Misri.
Yanga hawapaswi kubweteka wala kujiandaa kwa zima moto. Itaumbuka. Inapaswa kujua ina mechi ngumu kuliko hata ile ya Simba dhidi ya Zamalek ya nchi hiyo.
Nasema haya kwasababu kama ilivyokuwa kwa Simba, Yanga inakutana na Bingwa mtetezi wa michuno hiyo.
Pia inakutana na timu ambayo ambayo hapana shaka inafahamu namna gani Tanzania kuna timu nzuri zilizokusanya wachezaji mahiri.
Kama hivyo ndivyo; sidhani kama watacheza kwa kubahatisha. Wataingia uwanjani kutafuta ushindi katika mechi ya ugenini ili wapate nafasi nzuri watakaporudiana nyumbani kwao.
Wadau wa soka na mashabiki wataumia sana kama wachezaji na viongozi wao wataifananisha Al Ahly na Komorozine ya nchini Comoro.
Wataumbuka na kutoka vichwa chini. Nadhani ni wakati wao benchi laa ufundi kukaa chini na kuweka mipango kabambe.
Isiweke nguvu zao zote kwenye vichwa vya habari ili kuwavutia wadau wao juu ya mechi hiyo ngumu na inayoangaliwa kwa jicho makini sana.
Kwa bahati mbaya, timu zetu kongwe wakati mwingine hujikuta zinafungwa kabla ya mechi kumalizika.
Hii ni kwasababu wanajigamba tofauti na ufundi wao uwanjani. Angalia, wakati inashinda bao 7-0 dhidi ya Komorozine katika Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam, maofisa kadhaa wa Al Ahly walikuwapo uwanjani.
Al Ahly walikuwa wa kwanza kuwasoma Yanga kabla ya kujibu mapigo, ilipomtuma Mkwassa kuelekea Misri.
Wasiwasi wangu ni kwamba; Al Ahly walivuna vitu vingi kutoka kwa Yanga kwasababu ujio wao haukupewa mkazo tofauti na wao kujua kuwa Yanga wapinzani wao nao wangekwenda kwao kuangalia wanachofanya kabla ya mechi yao.
Kila mtu ana mbinu zake. Kinachotakiwa ni ushindi ndani ya uwanja, hivyo ni wakati wa Yanga kufahamu kiu ya mashabiki wa soka wa Tanzania kuona wanafuzu mbele ya Al Ahly.
Hili linaweza kufanikiwa, lakini si kwa kutoa tambo bila mikakati kwenye vyombo vya habari. Yanga kwa kupitia mabosi wake wa ufundi, wanapaswa wajuwe uwezo na hira pia wapinzani wao wanapokuwa uwanjani.
Mara kadhaa timu za Misri zinapoona zimeshindwa ndani ya uwanja hutafuta ushindi kwa mbinu nyingi, hasa kuwavuruga wapinzani wao kisaikolojia.
Hii iliwahi kutokea mara kadhaa na inaweza kutokea pia kwa Yanga, maana pamoja na ubora wa soka la Misri, bado hawana dharau kwa timu wanazokutana nazo, hasa za Tanzania.
Wachezaji wa Yanga waingie uwanjani kwa kutafuta ushindi mnono katika mechi ya kwanza nyumbani, kabla ya kutafuta sare, kama watashindwa kushinda tena uwanja wa ugenini.
Yanga ina kila sababu ya kusonga mbele dhidi ya Al Ahly, licha ya kuwa wanakutana na timu ngumu yenye kiu ya kusonga mbele.
Huu ndio ukweli, hivyo litakuwa jambo zuri kama kila mwana Yanga atakuwa na kiu moja ya kuona timu yao inasonga mbele kwa kufanya bidii uwanjani, kuandaa kikosi imara na sio kuwa wajuzi wa kupamba kurasa za magazeti maana soka la ainaa hiyo daima haliwezi kuwasaidia.


"Mungu ibariki Tanzania..."
 
yanga hana ubavu wa kuwafunga warabu tuache kufarijiana.mpira ni uwekezaji sio leo kuna mechi unaanza kutoa ahadi eti kila goli mtakalofunga nitatoa 50milioni
 
hawajatuzidi kila kitu tumewazidi majungu,kuamini ushirikina na mpira wetu kucheza magazetini
 
Hujui lolote we kiazi, ina maana hujui kama kocha msaidizi wa Yanga alikuwa Cairo siku chache zilizo pita?
 
"Kocha Msaidizi wa Al Ahly, Ahmed Ayoub ameichambua Yanga kwa kusema ni timu bora katika kushambulia, lakini si nzuri kwenye safu ya ulinzi."


Katika mahojiano na mtandao wa klabu hiyo, Ayoub alisema, ushindi wa jumla ya mabao 12-2 ilioupata Yanga dhidi ya Komorozine ni uthibitisho kwamba safu yake ya ushambuliaji ni moto wa kuotea mbali.
Katika michezo 17 ya Ligi Kuu Tanzania Bara safu ya ushambuliaji wa Yanga imefunga mabao 41 na kuruhusu mabao 12 hadi sasa.
“Yanga ina safu ya ushambuliaji yenye nguvu kwani imefunga mabao 12 katika raundi ya awali ya Ligi ya Mabingwa ilipocheza na Komorozine ambayo matokeo ya jumla ni 12-2,” alisema Ayoub.
Aliongeza: “Ina kikosi chenye nyota watano wa kulipwa kutoka Congo, Rwanda, Burundi na Uganda ambao wana mchango mkubwa katika safu ya ushambuliaji.”
Pamoja na kusifia safu ya ushambuliaji ya Yanga, kocha Ayoub alisema atatumia udhaifu wa ngome ya ulinzi kupata matokeo mazuri.
Alisema beki ya Yanga si imara kwani haina ushirikiano wa kutosha miongoni mwa wachezaji wake husika.
“Timu ya Tanzania ina udhaifu katika eneo la ulinzi ambako kimsingi hakuna muunganiko mzuri wa wachezaji wanaocheza eneo hilo,” alisema Ayoub.
Kocha huyo alishuhudia pambano la kwanza kati ya Yanga na Komoriozine lililopigwa kwenye Uwanja wa Taifa.
Kauli ya kocha huyo ni changamoto kwa Kocha wa Yanga, Hans Van Der Pluijm kwani ni wazi anatakiwa kuisuka kikamilifu ngome yake ya ulinzi kabla ya mchezo kati yake na vigogo hao wa Misri.
Safu ya ulinzi ya Yanga inaundwa na mabeki wa kati Kelvin Yondani na Nadir Haroub pamoja na mabeki wa pembeni Oscar Joshua anayecheza kushoto na Mbuyu Twite kulia.
Pluijm alisema, ana imani sasa kikosi chake kimeiva kisawasawa na kina uwezo wa kuisambaratisha Al Ahly yenye jina kubwa na historia ya kipekee barani Afrika.
“Timu yangu imeimarika, kwa sasa unaona kabisa jinsi tunavyocheza wachezaji wanajiamini na wanafanya kile ambacho mimi nimewaelekeza.”
“Katika soka kila kitu kinawezekana, kama Daudi aliweza kumshinda Goliath kwa nini isiwezekane kwa Yanga kuifunga Al Ahly? Hakuna linaloshindikana.”
Tangu 1982, mshambuliaji Omary Hussen anashikiria rekodi ya kuwa mchezaji pekee wa Yanga aliyefanikiwa kuzitikisa nyavu za Al Ahly hadi sasa katika mashindano yanayosimamiwa na Shirikisho la Soka Afrika(CAF).


mcl
 
Kuna kitu kinaitwa 'objective criticism' ambacho wengi hawajakizoea kwa sababu ni kusaidia kujenga kwa kukosoa. Nadhani ndicho ambacho vyombo vyetu vya habari na waandishi wake huwa wanajaribu kuvifanya. Ni kitu kizuri. Ila Watanzania wengi (nikiwamo mimi) huwa hawapendezewi na namna ukosoaji huo unavyofanyika. Huwezi kukosoa kwa kudharau na kukebehi. Anayekosolewa hatakuwa na moyo wa kusikiliza ama kusoma hata sentensi moja zaidi. Kwa hivyo hatafaidika na uhalisia wa kasoro zinazotolewa na mapenedekezo ya kuziondoa. Kibaya zaidi, anayekebehiw. Siye tu anayekosolewa, bali jamii nzima ya Watanzania. Chombo au mwandishi gani wa habari hapa kwetu asiyeikosoa Simba, Yanga, TFF, au taasisi yoyote kwa kuweka kauli 'Watanzania wana tatizo...... /Wangekuwa wenzetu wangefanya......./Kwa namna hiii Tanzania ita......../ Ndio maana Tanzania iko.......... Tujue kwamba hata hao tunaowaona wamepiga hatua kuliko sisi (ambao tumo kuiha kutoka kwao) wameanza karne ama miongo mingi kuliko sisi. Wana mazingira bora zaidi ya kiuchumi, kijamii na kimaendeleo kuliko sisi. Huwa nashangaa kulinganishwa Kaunda na Old Trafford, angalau sijasikia ikilinganishwa Azam Comlex na Alliance Arena. Hata hao tunaowatolea mifano ya ubora wana kasoro zao. Mara ngapi timu zetu zinapewa misukosuko tunapokwenda kucheza nao masindano huko kwao? Mara ngapi timu zetu zinaonewa waziwazi (ingawa waandishi wetu wanatetea zaidi wanapoona inaonewa Arsenal dhidi ya Bayern) na waamuzi, licha ya unaosemekana kuwa ni udhaifu wao?
Madhumuni ya utangulizi huu mrefu wa hoja yangu ni kukosoana bila ya kudharauliana wala kujidharau na kuwa tayari kukosolewa hivyo. Tanzania ni nchi adhimu mno na Watanzania ni watu muhimu mno wasiostahili kudhalilshwa kila tunapohitaji kukosoana. Ukiondoa udhalilishaji huo, naunga mkono hoja ya mtoa mada.
 
Mmeshanunua majembe kwenda kulima jumamosi?hatuwataki simba uwanjani jmosi,tickets zote za VIP ziuzwe kwenye matawi ya yanga.....wanajangwani wote tununue tickets tukawamalize waarabu....hamna haya kuiongelea Yanga,alafu mnanishangaza wakati juzi tu timu ilikuwa Turkey..mnataka matayarisho gani...jadili timu yenu mbovu wachezaji wanalia njaa na mnafungwa na hata kamgambo...
 
Mpira hauchezwi nje ya uwanja, dakika 90 zitaamua. Kikosi chao kilichokuja Tanzania hiki hapa:

الموقع الرسمى للنادى الأهلى

Tusiwaogope saaaaaaaaaaana, utafikiri huwa wako zaidi ya 11 uwanjani au hata kila mmoja ana zaidi ya miguu 2, matokeo ya mechi zao haya hapa:

الموقع الرسمى للنادى الأهلى


Kwa sasa siyo timu ya kutisha kihivyo, wamecheza mechi 8 za ligi, wana pointi 16 na magoli ya kufunga 10, kwa nini tuwaogope?


Kong'oli hapa: http://www.ahlyegypt.com/LeagueTable.aspx?pgid=13

Mashabiki wa Mikia njooni uwanjani Jumamosi, achaneni na kwenda kufyeka pori huko Bunju, mtashuhudia historia ikiandikwa uwanja wa Taifa.
 
Mpira hauchezwi nje ya uwanja, dakika 90 zitaamua. Kikosi chao kilichokuja Tanzania hiki hapa:

الموقع الرسمى للنادى الأهلى

Tusiwaogope saaaaaaaaaaana, utafikiri huwa wako zaidi ya 11 uwanjani au hata kila mmoja ana zaidi ya miguu 2, matokeo ya mechi zao haya hapa:

الموقع الرسمى للنادى الأهلى


Kwa sasa siyo timu ya kutisha kihivyo, wamecheza mechi 8 za ligi, wana pointi 16 na magoli ya kufunga 10, kwa nini tuwaogope?


Kong'oli hapa: الموقع الرسمى للنادى الأهلى

Mashabiki wa Mikia njooni uwanjani Jumamosi, achaneni na kwenda kufyeka pori huko Bunju, mtashuhudia historia ikiandikwa uwanja wa Taifa.
tupe na matokeo ya hivi karibuni katika michezo ya kimataifa?
 
unaweka Malink ambayo hata hayana uhusiano na unachopost, ma link yako yamejaa mapicha tuu

Tatizo letu waTZ ni wavivu wa kusoma. Matokeo yako hapo angalia vizuri utaona Ahly 3-2 CSS, ukishaona rudi hapa uombe radhi. Kwa taarifa yako hiyo ndiyo Official Website ya Al Ahly siyo kama timu fulani hivi; website haina lakini inajigamba kujenga uwanja wa mabilioni ya Shs ndani ya siku 100.
 
Yanga hata ikishinda hapa bado ushindi wao utakua mdg sn hakuna jeuri ya 3 au 2-0. Kama watapata goli zaidi ya 1 waarabu wanauwezo wa hata gol 1 ambalo litakua kiama kwa yanga. Hadhi za simba j/mosi kwenda kufyeka uwanja ni vichekesho na vituko vya mfa maji
 
Back
Top Bottom