Akiwa mahabusu Segerea, Mbunge Esther Matiko anunua bati 1324 kuezeka vyumba vya madarasa Tarime Mjini

Mwanahabari Huru

JF-Expert Member
Mar 9, 2015
14,243
34,899
Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini Mhe Esther N. Matiko ameamua kununua Bati zipatazo 1324 kwa ajili ya kuezeka Vyumba vya Madarasa 21, Ofisi 3 za Walimu na Vyoo 2 vyenye jumla ya Matundu 16. Mhe Esther N. Matiko ambaye ni Mbunge wa Jimbo la Tarime Mjini yuko Gerezani kwa muda wa siku 72 tangu kufutiwa dhamana na Mahakama ya Kisutu Jijini Dar es salaam.

Mhe Esther N. Matiko ameamua kuchukua maamuzi hayo baada ya idadi kubwa ya wanafunzi wa Darasa la 7 waliofaulu kujiunga na kidato cha kwanza wapatao *2046* kati ya hao ni Wanafunzi *416* tu walipata nafasi ya kuanza kidato cha kwanza na Wanafunzi *1630* wamekosa nafasi ya kujiunga kidato cha kwanza sababu tu ya upungufu wa vyumba vya Madarasa katika Shule za Sekondari Tarime Mjini.

Mhe Eather Matiko ameamua kununua Bati hizo kupitia fedha za Mfuko wa Jimbo ambazo ni Tsh *31,000,000/=* ili kuwezesha uezekaji wa Madarasa hayo na kutoa fulsa kwa watoto hao kupata Haki yao ya Msingi ya kupatiwa Elimu.

Bati hizo zilizonunuliwa na Mhe Bashiri Abdalah Suleiman (Sauti) ambaye amekaimu nafasi ya Mhe Matiko mgawanyo wake ni kama ifuatavyo.

(1) Shule ya Sekondari Sabasaba Mabati 440 kuezeka Madarasa 7 na Ofisi 1 ya Walimu na Matundu 8 ya vyoo

(2) Shule ya Sekondari Nyamisangura Mabati 240 kuezeka Madarasa 4 na Ofisi 1 ya Walimu

(3) Shule ya Sekondari Nyandoto Mabati 120 kuezeka Madarasa 2

(4) Shule ya Sekondari Kenyamanyori Mabati 142 kuezeka Madarasa 2

(5) Shule ya Sekondari Tagota Mabati 250 kuezeka Madarasa 4 na Ofisi 1 ya Walimu na Choo cha Matundu 8

(6) Shule ya Sekondari Nkende Mabati 190 kuezeka Madarasa 3

(7) Shule ya Sekondari Rebu Mabati 60 kuezeka Darasa 1.

Kukamilika kwa vyumba hivyo vya Madarasa kutakuwa kumetoa fulsa kubwa sana kwa Wanafunzi walioachwa kujiunga na elimu ya Sekondari ikiwa ni haki yao ya Msingi.

Ofisi ya Mbunge Jimbo la Tarime Mjini inapenda kuwaambia Wananchi wote wa Tarime Mjini kuwa Bati hizo zote zilizopelekwa kwenye Shule wanazojenga zimetolewa na Mhe Esther N. Matiko na sio Mtu yeyote wala Ofisi ya Mkurugenzi kama inavyosemwa na baadhi ya Watendaji wa Kata pamoja na baadhi ya Walimu Wakuu kwenye Shule hizo.

Mhe Esther N. Matiko anapenda kuwahasa Wananchi wote na watendaji waliopokea Bati hizo zitumike kwa Matumizi yaliyopangwa tu na sio jambo lingine.

Tarime Yetu Mshikamano Kwa Wote
Rasirimali Zetu Kwa Maendeleo Yetu

Imetolewa na:-
Peter Magwi Michael
Katibu wa Mbunge
Jimbo la Tarime Mjini
 
Pengine hizi ni zile fedha cdm waliyoipata walipobadili gia angani na kampeni za mabadiliko Lowasa. Ameamua arudishe kwa maskini kama njia ya kutubu.

Hii itakuwa ni fundisho kwa wengine cdm waige mfano huu wa kujisafisha. Dhambi ile wasipoitubu hakuna atakaye baki salama.
 
Pengine hizi ni zile fedha cdm waliyoipata walipobadili gia angani na kampeni za mabadiliko Lowasa. Ameamua arudishe kwa maskini kama njia ya kutubu.

Hii itakuwa ni fundisho kwa wengine cdm waige mfano huu wa kujisafisha. Dhambi ile wasipoitubu hakuna atakaye baki salama.

Unaongelea mambo ya kuhisi na kufikirika wakati tupo kwenye mgogoro wa 1.5 T?
Hizo na zile za escrow nani ametubu licha ya majina y awapokeaji kuwekwa hadharani? Mmoja akaamua kuzirudisha TRA, mbona hazikusikika kauli za aina hii?
 
Unaongelea mambo ya kuhisi na kufikirika wakati tupo kwenye mgogoro wa 1.5 T?
Hizo na zile za escrow nani ametubu licha ya majina y awapokeaji kuwekwa hadharani? Mmoja akaamua kuzirudisha TRA, mbona hazikusikika kauli za aina hii?

Huoni Matiko kajiunga na waina yake wakina singasinga na rugemalila. Hujui kuwa viongozi wa Escrow wako ndani kitambo?
 
Watu wasiojulikana wanatamani wakayatoboe hayo mabati kwa misumari ili kumkomoa Mh. Mbunge.
 
Naomba kujua ni utaratibu gani hufutwa kuidhinisha matumizi ya pesa za Mfuko wa Jimbo? Na inaudhi idhaa na nani? Na nani ni signatory wa pesa hizo?
 
Unajua maana ya katibu wabunge?? Je, Unafahamu kwamba wabunge wote wana makatibu kwenye ofisi zao ???
Ujinga ni utumwa wa elimu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Mbwiga umeusoma huo uzi na kuuelewa au umedandia treni kwa mbele na uharo!

Aliyeandika barua ndiye katibu akitufahamisha kaimu mbunge ni huyo Selemani sasa wewe na ulevi wako wa mbege hauelewi nini?
 
Back
Top Bottom