Akaunti ya vikundi

Akaunti ya vikundi

el mariachi

New Member
Joined
Mar 28, 2015
Posts
4
Reaction score
1
jamani wadau naomba mnisaidie kama kuna mtu anajua procedure za kufata ukitaka kufungua account ya kikundi CRDB, NMB au bank yoyote ile..
 
Nenda benki,lakini pia muandike muhtasali wa kikundi na sahihi zenu, pia sahihi ya mwenyekiti mtunza fedha(mhasibu) na katibu ndo zitakua zikitumika ktk kutoa pesa, zaidi wanakuja wataaram
 
Zingatia yafuatayo:

1. Muwe na shughuli ya kiuchumi
2. Kama hamzidi watu 20
3. Sajili jina la kikundi chenu brela
4. Andaeni muhtasari wa kikao cha makubaliano ya kikundi chenu ambapo kila mjumbe atatia sahihi.
5. Kikundi kiwe na viongozi- Mkiti, Katibu, Mhazini
6.Andikeni kwa Meneja wa Benk kuomba kufungua akaunti ya kikundi
6. Sema watia sahihi benki, na namna watakavyoweza kutoa pesa.
7. Ambatanisha nyaraka tajwa hapo juu, usajili, Tin, leseni.

Kazi rahisi, mwaweza kufanya wenyewe, kama mtahitaji msaada tuwasiliane ktk private box. Nawashauri mfungue akaunti Equity Bank Tanzania- hakuna mizegwe.
 
Sorry mkuu apo number 1 unamaanisha shughuli hiyo iwe ya kikundi or?
 
Back
Top Bottom