Ajira za WCF ni za kuangalia kwa umakini mkubwa

BABA TUPAC

JF-Expert Member
Sep 30, 2015
1,527
3,810
WCF ni Workers Compensation Fund, office zao zipo Dar es Salaam- Victoria (Jengo la GEPF)

1. Jumamosi ya tarehe 18 March mliita applicants kufanya Interview katika post mbali mbali pale IFM

2. Tunafaham fika kuwa kuna vijana wanafanya internship katika karibia nafasi zote mlizozitangaza

3. Nafasi zile zilizotangazwa hazikuwa Internal, kwa maana ya kwamba hazikuwa ni nafasi za watu wa ndani

4. Tunataka haki itendeke, kama hao intern wenu watafeli interview waachwe na endapo wakifaulu wachukuliwe

5. Hatutegemei kuona mnawachukua intern peke yao na kuwaacha watu waliotoka Kigoma kuja dar kufanya interview na wakafaulu

6. Majina yote ya intern tunayo hivyo mkiwapa ajira kwa upendeleo tutasambaza majina yao kama tulivyofanya majina ya wale waliopendelewa nafasi za uhamiaji kipindi kile

7. Msipokuwa makini, hizo nafasi za kazi zitaondoka na watu hapo ofisini kwenu.

Taarifa hii, watumieni wafanyakazi wa nafasi za juu wa WCF. Waambieni wakicheza tu, itakula kwao. TUNAWAANGALIA KWA UMAKINI MKUBWA
 
Mkuu point yako iko vizuri ila tatizo ni kwamba mna uhakika kilwa wale interns wao walishindwa interview??
Hii nchi kuna vitu huwa vinaenda kwa kujuana inaitwa kamlete afu kamawaloweza kupata internship kwa nini wakose ajira maana hata hizi kuzipata tu mbinde
 
We vipi? Unatuandikia vifupisho WCF ndo nini? Umeitwa kwenye interview ya Water Closet Foreman (WCF) halafu ndo unatoa vitisho hivo? Ebo!
 
Mimi nashangaaa Sana, mitihani yenyewe ilikua kujaza tutlis paper na kusahihisha kwa mashine nashangaaa hadi leo hawatoi majibu sijui wanachakachua nn huko,
 
Mtoto wa mjomba.. Ajira ni kujuana wewe huoni hata rais wako?
Anatamani ajira zote za tz zipitie kwake.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom