Ukweli lile tangazo zilikuwa siasa , kwanini ??. Kwasababu waziri alijikuta anatoa tangazo lile bila kutarajia baada ya serikali ya Zanzibar kitoa tangazo kuwa inatazamia kuajiri walimu 15000 ambao ni wazanzibar tu ikiwa ni muendelezo wa kuionesha Tanganyika kuwa cha Zanzibar ni cha Zanzibari na watanganyika hakiwahusu .
Sasa ili kufunika panic za watanganyika ( Tanzania bara kama mnavyojiita ) juu ya swala la ajira katika mambo ya muungano waziri wenu nae akasimama majukwaani na kutoa tangazo kuwa serikali ya Tanganika inatizamia kuajiri walimu na madaktari 25, 000 ndani ya mwaka huu ikiwa uwezo huo haona ,na huku ikiwa imeshikwa na aibu kuona nchi ndogo ya Zanzibar inaajiri watumishi 15000 afu huku lijinchi lenye watu wapatao milion 60 lina ajiri watu 25000 tu .
Lakini itakumbukwa kuwa katika ajira hizo 25000. Asilimia 10% au 15% ni za wanzanzibar .
Swali je , katika ajira hiza 15000 je ni asilia ngapi za watanganyika ???
Je , swala la ajira linazungumziwaje kwenye muungano , ni sehemu ya muungano au la ??