Ajira ya muda katika Jamii Media - Afisa Mawasiliano (Lindi)

Jamii Opportunities

JF-Expert Member
Feb 10, 2014
4,814
1,524
Tulishawahi kutangaza nafasi kama hii kwa majimbo mengine 9 (tembelea - Ajira ya muda katika Jamii Media - Afisa Mawasiliano (9))

TANGAZO LA AJIRA YA MUDA - AFISA MAWASILIANO (Lindi)

1. UTANGULIZI

Jamii Media ni Kampuni gwiji inayojishughulisha na taarifa na habari kwa kupitia Mitandao ya Kijamii. Kampuni hii inachochea Uhuru wa Kujieleza, Uwazi katika Utawala, na Uwajibikaji kupitia Mtandao wao maarufu uitwao JammiForums.com.

Jamii Media pia inamiliki na kuendesha jarida-mtandao liitwalo FikraPevu.com na kusimamia kurasa zenye wasomaji wengi kwenye mitandao ya Kijamii kama Twitter, Facebook na Instagram.

2. CHIMBUKO

Jamii Media inatarajia kuanza utekelezaji wa Mradi utakaofahamika kama “TUSHIRIKISHANE PROJECT” Lengo la Mradi huu ni kuwawezesha wananchi na kuimarisha ushirikiano kati ya wananchi, wawakilishi wa kuchaguliwa (hususani Wabunge) na Uongozi wa Wilaya.

Tushirikishane utakuwa Mradi wa miezi kumi na miwili utaotekelezwa kwenye Majimbo tisa (9), ya Uchaguzi na utashirikisha Wabunge tisa (9), Madiwani wa kata katika Majimbo husika, watumishi wa Halmashauri katika majimbo husika na wananchi wa maeneo utakapotekelezwa mradi huu.

Lengo mahsusi la kuhamasisha ushirikiano kati ya wadau wakuu wa mradi huu ni kuharakisha/kurahisisha utekelezwaji wa ahadi za viongozi wa kuchaguliwa, kuchochea ufanisi wa Serikali Wilayani katika kutoa huduma za jamii hususani kwenye Sekta za afya, maji, elimu na mioundombinu. Na mwisho, kuweka mfumo wa kuongeza msukumo wa uwajibikaji wa viongozi kwa wananchi.

Ili kufikia azma hii, ni muhimu wananchi kuwa na uelewa juu ya rasilimali zilizopangwa kwa ajili ya maeneo yao, lazima wajue mipango ya Serikali kwenye ngazi ya Wilaya zao. Uelewa huu unapatikana kwa wananchi kuwa na fursa ya kupata taarifa tena zikiwa katika mfumo ambao ni rahisi kueleweka.

Kwa bahati mbaya kwa sasa taarifa nyingi zinazowagusa wananchi hazipatikani kirahisi na haziko katika mfumo rahisi wa kueleweka na wengi. Jambo hili linalotoa nafasi kwa baadhi ya watu kutumia taarifa kwa manuaa binafsi ikiwemo kuwahada wananchi wakati wa kuomba uongozi. Mradi wa Tushirikishane ungependa kuziba mwanya huu kwa kuhakikisha wakati wote wananchi wanapata taarifa kwa wakati na katika jinsi ambayo zinaeleweka kwa urahisi.

Ili kutekeleza mradi huu kwa ufanisi, Jamii Media imetengeneza nafasi za AFISA MAWASILIANO kwa kila Jimbo litakaloshiriki kwenye Mradi. Maombi yanakaribishwa kutoka kwa watu wenye vigezo wanaoishi kwenye majimbo yafuatayo:

1. Bunda
2. Arumeru Mashariki
3. Amani, Zanzibar
4. Bukoba mjini
5. Kigoma mjini
6. Kigamboni
7. Lindi
8. Nzega
9. Sengerema
10. Lindi

3. VIGEZO VYA MUOMBAJI
- Awe mkazi aliyeshiriki kupiga kura kwenye Jimbo analoomba kuwakilisha na maskani yake ya sasa iwe Jimboni.
- Awe na taarifa za kina kuhusu ahadi za wagombea wa nafasi za ubunge kutoka uchaguzi uliopita na asiwe na upendeleo
- Awe na uwezo wa kuchambua mambo na taarifa pasipo kuathiriwa na itikadi, mapenzi binafsi au upendeleo wa aina yoyote
- Awe na elimu ya kidato cha nne na kuendelea na ajue kukusanya habari, kuandika taarifa na kufuatilia majibu ya malalamiko au maoni ya wananchi kwa viongozi wa umma.
- Awe mtumiaji mzuri wa mawasiliano ya kisasa hasa mitandao ya kijamii. Na awe mshiriki hai wa mijadala mbalimbali inayogusa jamii.
- Muombaji aliyejisajili na kuchangia mijadala mbalimbali ya JF kwa muda zaidi ya miezi sita ana nafasi pekee

4. JINSI YA KUTUMA MAOMBI

Watu wote wanaohisi wanakidhi vigezo vilivyorodheshwa hapo juu watume maombi yao kwa njia ya barua-pepe wakijibu maswali yafuatayo:

· Jina lako kamili, anwani yako na
· Ahadi gani zilitolewa na Mbunge wako wa sasa? Taja walau tatu
· Hali ya huduma za kijamii ikoje katika Jimbo unalotaka kuwakilisha?
· Vipaumbele vya Serikali katika Wilaya yako ni vipi?

Majibu yatumwe kwenda vacancies@jamiiforums.com na kwenye kichwa cha habari andika JINA LA JIMBO unalotaka kuwakilisha likifuatiwa na neno AFISA MAWASILIANO. Mfano: UBUNGO—AFISA MAWASILIANO.

Kazi hii itakuwa ya mkataba wa miezi minane (8) kuanzia Julai, 2016 na itamhitaji mhusika kuzunguka katika kata mbaimbali za Jimbo kukusanya taarifa na matukio.

Mwisho wa kutuma maombi na Julai 9, 2016.
 
Bado hawajaitwa Mkuu,

CV ni nyingi sana, hivyo zinahitaji kupitiwa taratibu na kwa umakini. Team ya Jamii Media itatembelea majimbo hayo yote ndani ya wiki nane (8) zijazo. Interview zitafanyika kwa tarehe tofauti kwa kila jimbo kwenye jimbo husika.

Hata hivyo inasikitisha sana kuona vijana wetu wasivyokuwa makini katika masuala ya msingi na makini. Watumaji wengi wametuma taarifa nusu nusu na hawajafuata maelekezo na taratibu zinazotakiwa katika kutuma maombi hayo. Hata hivyo tunashukuru kwa wale ambao wametimiza vigezo hivyo (ingawa ni wachache waliofaulu katika hilo).

Zile nafasi za mwanzo washaitwa kwaajili ya interview?mana kuna dogo langu alia apply
 
Bado hawajaitwa Mkuu,

CV ni nyingi sana, hivyo zinahitaji kupitiwa taratibu na kwa umakini. Team ya Jamii Media itatembelea majimbo hayo yote ndani ya wiki nane (8) zijazo. Interview zitafanyika kwa tarehe tofauti kwa kila jimbo kwenye jimbo husika.

Hata hivyo inasikitisha sana kuona vijana wetu wasivyokuwa makini katika masuala ya msingi na makini. Watumaji wengi wametuma taarifa nusu nusu na hawajafuata maelekezo na taratibu zinazotakiwa katika kutuma maombi hayo. Hata hivyo tunashukuru kwa wale ambao wametimiza vigezo hivyo (ingawa ni wachache waliofaulu katika hilo).
mitanzania ndio tulivyo kufollow instruction ni mtihani kwetu
 
Madhara ya elimu ya mwendokasi yanajidhihirisha kila kona. Ikiwa kufuata melekezo madogo tu ni mtihani, ni vipi tutafanikiwa kwenye mageuzi ya Viwanda!?
 
Bado hawajaitwa Mkuu,

CV ni nyingi sana, hivyo zinahitaji kupitiwa taratibu na kwa umakini. Team ya Jamii Media itatembelea majimbo hayo yote ndani ya wiki nane (8) zijazo. Interview zitafanyika kwa tarehe tofauti kwa kila jimbo kwenye jimbo husika.

Hata hivyo inasikitisha sana kuona vijana wetu wasivyokuwa makini katika masuala ya msingi na makini. Watumaji wengi wametuma taarifa nusu nusu na hawajafuata maelekezo na taratibu zinazotakiwa katika kutuma maombi hayo. Hata hivyo tunashukuru kwa wale ambao wametimiza vigezo hivyo (ingawa ni wachache waliofaulu katika hilo).
Afadhali waliotuma vizuri ni wachache,hao wengine wameonyesha kuwa kazi awataiweza.
 
Bado hawajaitwa Mkuu,

CV ni nyingi sana, hivyo zinahitaji kupitiwa taratibu na kwa umakini. Team ya Jamii Media itatembelea majimbo hayo yote ndani ya wiki nane (8) zijazo. Interview zitafanyika kwa tarehe tofauti kwa kila jimbo kwenye jimbo husika.

Hata hivyo inasikitisha sana kuona vijana wetu wasivyokuwa makini katika masuala ya msingi na makini. Watumaji wengi wametuma taarifa nusu nusu na hawajafuata maelekezo na taratibu zinazotakiwa katika kutuma maombi hayo. Hata hivyo tunashukuru kwa wale ambao wametimiza vigezo hivyo (ingawa ni wachache waliofaulu katika hilo).
Kwahyo kwa sasa ni za Lindi tu...au hzo za sehemu nyngn tunaweza apply pia..mana mm npo kigamboni nlichelewa kuona tangazo
 
Mkuu,

Wewe sasa jukumu lako itakuwa kufuatilia endapo hayo majimbo tunayoanza nayo yataweza kufikisha malengo ya mradi. Kufanikiwa kwa mradi huu ni fursa ya mradi huo kupanuliwa kwenda majimbo mengine mengi.

Aisee mie nipo jimboni kwa pm sipati hii fursa?
 
Mkuu,

Ninashauri utume tu. Siwezi kujibu kama itapokelewa ama lah. Tokana na changamoto ya waombaji wengi kutotimiza vigezo, pengine ukabahatika.

Kwahyo kwa sasa ni za Lindi tu...au hzo za sehemu nyngn tunaweza apply pia..mana mm npo kigamboni nlichelewa kuona tangazo
 
Mkuu FisadiKuu,

Shindano hilo tulifanya kwa kushirikiana na China Radio International. Tokana na matatizo yaliyo nje ya uwezo wetu, hizo simu hadi sasa hazikufika. Hivyo tulikuwa tunavuta muda kuhakikisha tusinunue na zikawasili. Hata hivyo Management ya Jamii Media imesha amua kununua simu hizo na hivyo zitawasilishwa wakati wowote.

Ninamkaribisha JamiiForums atoe taarifa kwa washiriki wote na washindi wote na kuahidi kwamba simu hizo zitakuwa tayari makao makuu kufikia Jumatatu ya tarehe 11 July, 2016.

Pole kwa usumbufu wote ulitojitokeza katika zoezi hili. CC: Nifah

Haa. Mi nataka kuomba Bunda. Sasa ndugu yangu nimepatwa utata kuandika ahadi maana Bunda kunamajimbo mawili Bunda mjini na Bunda vijiji sasa sijui mnakusudia jimbo lipi. Bunda vijijini mb ni Bonophace Mwita Getere na mjini ni Esther Amos Bulaya. Usichanganye na Mwibara kwa Alphaksad Kangi Lugola.. Note wilaya ya Bunda inamajimbo matatu.

CC #Jamii Jobs
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom