Ajira mpya za madaktari kutoka mwezi Mei

Interest

JF-Expert Member
Apr 11, 2015
3,434
7,069
Serikali imesema inatarajia kutangaza Ajira mpya za Madaktari kuanzia Mwezi Mei mwaka huu na kuwasambaza maeneo mbalimbali yenye uhitaji.

Ahadi hiyo ilitolewa na Waziri Angela Kairuki akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Njombe akifuatana na kamati ya kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.

Ingawa hakutaja Idadi ya nafasi za ajira zitakazotolewa kwa madaktari, wiki iliyopita Mganga Mkuu wa Serikali Prof Kambi na Waziri wa Afya Ummy walizungumzia suala la uhaba wa madktari ambapo ilielezwa kuwa idadi ya madaktari wanaohitajika nchini ni 3,510.

Waziri Ummy alifafanua kuwa kuna upungufu wa 49% ya wataalamu wa afya hususan madaktari katika hospitali za umma, vituo vya afya na zahanati.

Hapo chini nimeiweka taarifa hii kwa kina kama ilivyoandikwa na gazeti la Nipashe..

=========

WAZIRI ANGELLAH KAIRUKI.jpg


SERIKALI imesema inatarajia kutangaza ajira mpya kwa madaktari Mei, mwaka huu na kuwasambaza katika maeneo mbalimbali yenye uhitaji.

Ahadi hiyo ilitolewa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora), Angela Kairuki jana akiwa katika ziara ya siku mbili mkoani Njombe, akifuatana na Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za Mitaa.

Kamati hiyo ilitembelea Hospitali ya Makambako ambayo inajenga chumba cha upasuaji na wodi ya kinamama na watoto.

Waziri Kairuki alisema serikali itapeleka madaktari katika Hospitali ya Makambako kulingana na maombi yao katika ajira ambazo zitatolewa na serikali Mei.

Alisema eneo la Makambako linahitaji madaktari wa kutosha kutokana na ajali nyingi zinazosababishwa na kuwa mapitio ya magari kutoka maeneo ya mikoa ya Njombe, Ruvuma na Mbeya.

Ingawa Kairuki hakutaja idadi ya nafasi za ajira zitakazotolewa kwa madaktari, lakini wiki iliyopita,

Mganga Mkuu wa Serikali, Prof. Muhammad Kambi na Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, walizungumzia suala la uhaba wa madaktati.

Prof. Kambi alisema idadi ya madaktari wanaohitajika nchini ni 3,510 na katika idadi hiyo, mahitaji zaidi yapo kwenye hospitali za wilaya wanakohitajika madaktari 832, za rufani (460), vituo vya afya (816), Bugando (152) na Hospitali ya Taifa Muhimbili madaktari 235.

Nyingine ni KCMC (143), hospitali za rufani za mikoa (460), madaktari 111 katika Taasisi ya Mifupa Muhimbili (MOI), Hospitali ya Ocean Road (57), Mirembe (37), CCBRT (26) na Rufani Mbeya (106).

Naye Waziri Ummy alisema kuna upungufu wa asilimia 49 ya wataalamu wa afya hususani madaktari katika hospitali za umma, vituo vya afya na zahanati.

Ummy alisema uhaba wa madaktari unaikabili zaidi mikoa ya Simiyu, Shinyanga, Kigoma, Mara, Simiyu, Kagera na Rukwa na kuwa hautokani na uchache wa madaktari, bali uwezo wa kuwaajiri wote kwa wakati mmoja. Alisema uwezo wa serikali ni kuajiri madaktari 400 kila mwaka.

Miaka michache iliyopita uwezo wa serikali wa kutoa ajira mpya kwa watumishi ulishuka na miongoni mwa sekta zilizoathirika zaidi ni afya.

Hali hiyo iliendelea baada ya Machi mwaka jana serikali kusimamisha ajira mpya, uamuzi ambao ulithibitishwa rasmi na Rais John Magufuli Juni 22 wakati wa maadhimisho ya miaka 50 ya kuanzishwa kwa Benki Kuu ya Tanzania (BoT).

Rais Magufuli alisema mbali na kusimamisha ajira mpya. pia upandishaji wa madaraja umesimamishwa na kuwa lengo la hatua hiyo ni kupisha uhakiki wa watumishi hewa na vyeti.

ZIARA YA KAMATI
Kamati hiyo ikiwa mjini Makambako ilitembelea majengo mawili ya upasuaji na wodi ya kinamama yanayojengwa na Halmashauri ya Njombe na kuridhishwa na maendeleo ya ujenzi huo.

Mwenyekiti wa kamati hiyo, Jasson Rweikiza, alisema kutokana na juhudi zinazofanywa na Halmashauri hiyo, atakwenda kuisemea serikalini ili kuhakikisha kuwa huduma ya afya inapatikana kutokana na umuhimu wa mji wa Makambako.

Alisema kuwa mji wa Makambako una barabara nyingi ambazo zinapata ajali mara kwa mara na chumba cha upasuaji kitakuwa muhimu kwa kuwahudumia watu watakaopata ajali maeneo hayo.

“Kutokuwapo kwa chumba cha upasuaji ni kuwanyima watu haki ya kupata huduma ya afya, tutakachokifanya ni kuihimiza serikali kuharakisha ujenzi wa chumba hicho,” alisema Rweikiza.

Mbunge wa Kilolo, Venance Mwamoto, ambaye pia ni mjumbe wa kamati hiyo, alisema wakazi wa
Makambako watarajie makubwa kwa kuwa ujenzi utahamasishwa ili ukamilike haraka.

“Kwa kuwa hospitali hii inahudumia wakazi wengi kutoka baadhi ya halmashauri za mikoa ya Iringa, Mbeya na Njombe, hospitali hii ni muhimu sana kwa jamii,” alisema Mwamoto.

Mganga Mkuu wa Hospitali ya Makambako, Charles Mbota, alisema inategemewa na wakazi wengi na huduma ya upasuaji wamekuwa wakiifuata katika hospitali binafsi ambako gharama ni kubwa.

“Kama huduma hiyo ikipatikana katika hospitali ya mji, watakuwa na unafuu wa gharama,” alisema Dk. Mbota.

Chanzo: Nipashe
 
huyu mama anajisikiaje anavyodanganya mara kwa mara, bungeni alisema mwezi wa nne sasa anakwambia tena mwezi wa tano, baada ya hapo sijui atasemaje, hii serikali ni ya kipuuzi sijapata kuona.
 
Sijawahi kuona mtu mwenye kauli za kipuuzi na zisizotekelezwa kama huyu mtu.
Sijui anakumbuka tangu apewe uwaziri amesema kauli ngapi na kazitekeleza ngapi?
 
Huyu mama simpendi kwa sababu ya kauli za uongouongo.Mara ajira mpya,Mara uhakiki shame on u mama.
 
Maskini misukule ya magufuli, hawana pesa ila anatamani kuajiri, uwezo hawana, wamebajiza matamko tu ....... madaktari mlioko Tanzania njooni tufanye kazi Kenya, achaneni na porojo za magufuli, hata msipoletwa katika ajira 500 za kenyattra njooni binafsi Kenya moja moja achanane na madalali hao wanaotaka mjikomiit mkatwe 15% na mapato

Kenya ukifika utajisajili ndani ya siku 3 utapata leseni na unaenda wizarani kupangiwa kazi
 

Attachments

  • PRESS RELEASE - REGISTRATION RECOGNITION FOR EAC PARTNER STATES DOCTORS.pdf.pdf
    396.5 KB · Views: 45
Japo ana bla bla na mm sipo katk sekta ya kutumwa lakin namkubali sana huyu wazir,,,mzur balaa ila angekua modo kidgo angetisha zaid,,hakuna wazir wa kike mzur kama yeye east africa na central afrika
 
Kwa huu uongoz wa chama cha majambazi? Washindwe kuajiri makada wa ccm waajiri madaktari.
Hii ndiyo nchi ya vi-wonder. Hapa hakuna lolote na ni uongo mtupu.
Nchi inaendeshwa kwa kiki. KWA UONGOZI DHALIMU KM HUU HIYO HAITAWEZEKANA. Maajabu ya tz halafu bado wanawataka watu wawe wazalendo? Bila kuiondoa ccm madarakani hakuna maendeleo tena na hapo kutokuajiri watu wanaona raha
 
Hii nchi ina uhaba mkumbwa mno wa wauguzi kuliko madaktari lakini cha ajabu wauguzi hawaajiriwi na medical attendant wanafanya Kazi ya uuguzi wakati hawajasoma uuguzi na hawana license za uuguzi. Ama kweli nchi hii ni ya Vi wonder!!
 
Si mara ya kwanza taarifa za matumaini ya ajira kutolewa na huyu mama. Kumuamini sana sio ishu kwa sasa...
 
Back
Top Bottom