Ajira kwa Vijana

Ajira kwa Vijana

ameline

JF-Expert Member
Joined
Jan 8, 2013
Posts
2,292
Reaction score
1,152
Naomba mnisamehe kwa thread zangu za mara kwa mara huku jamani, natanguliza samahani,....
naomba niwapongeze wale vijana wote ambao wanaendelea kujikomboa kifikra na kujitambua hasa katika masuala haya ya ajira, roho inaniuma sana maana na mimi ni mhanga wa hili suala thats why huwa sichoki kulizungumzia kwa namna yoyote ile..nimepokea email nyingi sana wale ambao hamjajibiwa muwe wavumilivu tu nitawajibu kadri nitakavyoweza.

kwanza nimeshawasamehe wale woote walionitukana kwenye email baada ya kunyimwa kutukana hapa jf wakaamua kumalizia hasira zao kule kwenye amelinechao@gmail.com.ni changamoto tu katika maisha, ila baadhi yao baada ya kuwasomesha kwa hoja wamerudi na kuomba msamaha.

Napenda kuwatia moyo vijana wenzangu kuwa kile unachokiamini kinawezekana kwani baada ya kuwaandikia ile thread ya shukrani zangu kwenu, ni baada ya kuwapata vijana wawili wa degree ambao walijitoa kweli kufanya kazi yoyote kwa jitihada zangu nikawasaidia msichana yupo sheli na mvulana yupo arusha sundries kama store kipa, jana tena jumapili nimepata dada mwingine,humuhumu jf anatokea dar ila ana ndg huku ,amepata kazi kwenye kampuni inayoitwa sameer akiwa kama muuzaji msaidizi wa spare za magari,amesoma BBA mshahara 145,000/= huyu naye nimemuomba aje huku jf kuwashuhudia wanajf kinachoendelea huko aliko.

ndg wanajf na vijana wenzangu tunaotafuta ajira,msijikweze kutokana na elimu zenu mlizonazo huku mkiumia nafsini mwenu kwa kuogopa aibu au kushushwa thamani na rafiki ndugu au hata class mate wenzako! ukiwa unasubiri ajira ni bora ukajitoa kama vijana wenzako hawa kuhangaika kutafuta shughuli yeyote ya kufanya ambayo ni halali ambayo huvunji sheria za nchi ili ikusaidie kupunguza ukali wa ugumu wa maisha.kwa wale kaka zangu hata dogo hapo home akikuomba 200 ya nauli basi usipepese macho, na wale wadogo zangu na wadada wenzangu ni aibu kuomba hata hela ya kununua pads, au hata poda jamani,...

Naahidi kuendelea kuwasaidia vijana wenzanu kadri nitakavyoweza sina uwezo wa kifedha jamani, ila nitatumia akili yangu na maarifa Mungu aliyonijalia kuhakikisha kwamba hakuna msomi atakadhalilika kwa kuombaomba hovyo au kutukanwa kisa eti hana hela au hana kazi, maana wazazi wengine najua wanauliza maswali sana kwa siku hizi ambazo unasubiri ajira,kama mtu utajikweza eti msomi kufanya kazi yeyote ni kujidhalilisha naomba usicomment au usiandike lugha yeyote ya matusi au usinitumie email kunitukana bora ukae kimya uwaache wale ambao wanaona inawasaidia wasaidike.
email zenu nitawajibu nanitaendelea kuwajulisha pale opportunity zinapopatikana. Ahsanteni sana Mungu awabariki na awape majibu kule mlikotuma application basi mfanikiwe, na nafasi yeyote ikipatikana basi fanyeni. mwaaa!
 
umewapata maboyaaaa kijana na asante zako za kashifa.... jiangalieee:israel:
 
Mnatuvunja moyo ambao tunatangaza hapa waje ambao wanaajiriwa bila kujuana!!
 
umewapata maboyaaaa kijana na asante zako za kashifa.... jiangalieee:israel:

mmmh sijakupata kaka yangu,.ila waache haohao maboya wenye uhakika wa kuishi, hawaibi, hawaombi ila wanajikwamua wakizisubiri ajira zao hizo,nipo seriouse brother sichekeshi wana kufurahisha watu huku jf.
 
Mnatuvunja moyo ambao tunatangaza hapa waje ambao wanaajiriwa bila kujuana!!

elezea jinsi unavyovunjwa moyo mpendwa positive, just be open,usiweke wazo la kuajiriwa kwa kujuana kichwani Mungu ndiye anakujua wewe kwenye hizo nafasi, endelea kupigana tu siku yako itafika...
 
Back
Top Bottom