Ajilipua ndani ya msikiti Saudia

Ajilipua ndani ya msikiti Saudia

Gambamala

JF-Expert Member
Joined
May 13, 2014
Posts
1,045
Reaction score
766
[h=1]Ajilipua ndani ya msikiti Saudia[/h]
150522114350_saudi_arabia_mosque_attack_640x360_epa_nocredit.jpg


Mlipuaji wa kujitolea muhanga amejilipua ndani ya msikiti wa madhehebu ya Shia katika mkoa wa mashariki wa taifa la Saudi Arabia na kusababisha madhara makubwa.


Kulingana na vyombo vya habari nchini humo.
Mtu mmoja aliyeshuhudia alikiambia chombo cha habari cha Reuters kwamba kulikuwa na mlipuko mkubwa katika msikiti wa Imam Ali katika kijiji cha al-Qadeeh.
Amekadiria kwamba kuna majeruhi 30 katika shambulizi hilo ambapo zaidi ya watu 150 walidaiwa kusali ndani ya msikiti huo.

141215174201_mecca_mosque_saudi_arabia_640x360_getty_nocredit.jpg



Picha za runinga ya kundi la Hezbolla al-Manar zilionyesha vioo vilivyovunjika pamoja na vifusi ndani ya msikiti.
Miili iliozibwa na nguo ilionekana imetapakaa katika sakafu ya msikiti huo.


Watu wa dhehebu la Shia walio wachache wanaishi mkoa wa mashariki na kumekuwa na malalamishi ya washia wanaotaka kupewa haki zaidi.


Hili ni shambulizi la kwanza lililotekelezwa katika msikiti wa Shia.

141211134850_saudi_mosque_640x360_bbc_nocredit.jpg



Tukio hilo linajiri huku muungano wa majeshi unaoongozwa na Saudi Arabia ukiendeleza kampeni yake dhidi ya waasi wa kishia katika taifa jirani la Yemen.


Taifa la Saudi Arabia pia limetishwa na Islamic state ambalo linalengwa na muungano wa kimataifa iwemo ufalme huo wa kisunni

Source:BBC Swahili
 
Yaani sijui tunakoelekea, sijui tunataka nini yarabi, wa tz tuendeleze amani tuliyonayo.
 
Wewe mbona hueleweki picha za mlipuko zipo wapi kama hunamada katafute buyu ukune
 
Ni bora wameanza kulipua wao kwa wao labda wanaweza kupata akili
 
Waislam wanadai haki kutoka kwa waislam...dunia ingekuwa inatawaliwa na mataifa ya waarabu dunia sijui ingekuwaje,mungu aliona mbali
 
Sasa Freemason wanafosi kiama duh lakini nahamini kwa uwezo wa Allah watashindwa
 
Back
Top Bottom