Ajali za kila siku, nani mchawi wetu?

Ajali za kila siku, nani mchawi wetu?

Lekakui

JF-Expert Member
Joined
Apr 2, 2012
Posts
1,451
Reaction score
589
Ndugu wana JF,

Leo nimeona nije na topic ya hizi ajali za kila siku tusaidiane. Hivi tatizo liko wapi? Data zinaonesha bara la Africa lina asilimia 2 tu za magari yote duniani, lakini ajali ni asilimia 60 ya ajali zote duniani zinazotokana na magari.

Swali: Ikifika Africa tukawa na asilimia 4, je, ajali zitakuwa zaidi ya asilimia 100?

Nawasilisha
 
Tatizo sheria na kanuni za uendeshaji wa magari hazi zingatiwi na waendesha magari
 
Madereva wapate mafunzo yakinifu tuache porojo, leo ghafla kagua leseni nchi nzima, magari mengi yatakosa waendeshaji, wengi wetu wababaishaji..
 
Hatununui magari mapya tunanuna magari chakavu sana, mpaka "4th hand". Wenzetu wakiyatumia tu miaka mitano wanayauza.
 
Tatizo ni barabara mbovu na huu ubovu umechangiwa sana na waziri wa barabara John POMBE Magufuli.Barabara zina mashimo,zina michepuko na kona mbaya.Mchawi ni serikali chini ya usimamizi wa Magufuli.
 
Back
Top Bottom