Ajali za bodaboda ni hatari sana

Manyanza

Platinum Member
Joined
Nov 4, 2010
Posts
20,326
Reaction score
49,038

Ni ajali mbaya sana kuishuhudia na sijui hawa madereva kwanini huwa hawako makini na huwa hawafuati taratibu barabarani
 
Kazi ya Mungu haina makosa.

sidhani hapa kuna kazi ya Mungu mkuu, hawa jamaa wa bodaboda huwa hawako makini katika kazi zao na wanapenda sana kuchomekea, mfano ukiangalia mwendesha bodaboda akiwa kwenye mataa anapokua anajiendea bila kuangalia taa kama zinamruhusu apite au aendelee na safari lakini yeye hua hajali anajiendea tu
 
bora nlikuwa sipo kwenye kula nyama, mwili umesisimka, inatisha sana, bora nipande kibajaji kuliko hii kitu aisee, naogopa
 
Duh, hiyo picha haifai aisee, weka warning mtu afungue keshajiandaa!
 
hiv mnavyopenda kusema kazi ya mungu mnataka kutuaminisha kwamba mungu ni muuaji.wakati mwingine huwa mnakufuru sijui ni makusudi au ni bahati mbaya.
 
Hivi huyu sio yule jamaa aliyegongana na Fuso Morogoro? maana niliona ile picha ya fuso kwa jinsi ilivyobonyea pale alipogonga bodax2 utadhani mtu alipiga na nyundo.....Duh!!!😛hone:
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…