Ajali ya Tabata Matumbi: Nani dereva mzembe hapa?

Abd M

Member
Dec 19, 2015
23
9
241a624ad16e05da45ee8cebb833732d.jpg
 
Dereva wa lorry la mchanga ndio mwenye makosa. Sijui alikuwa anataka kupiga U-Turn
 
aisee sio siri jeshi la usalama.barabarani yatakiwa kifanyike kitu haraka sana.kama hawawezi kubadilika na.kufanya mabadiliko ya kutulinda raia wake basi waachie hizo nafasi aisee.

xishikwe na watu wenye maono na mbinu mpya.sheria zimekuwa hazifuati watu wanavunja sheria na kufanya watakavyo ya kugarim uhai wa raia wema.

watu wanafanya upuuzi sana kwa kuwa sheria hazina meno.mtu anafanya upuuzi wa kuchomekeana kama hivyo na kugarimu maisha ya raia wema na kuwatia vilema.vya maisha pasipo sababu.

kwanza huyo dereva wa roli unamfungia leseni yake maisha asiendeshe tena gari.then kifungo nae lazima kimhusu tena cha maisha.

maana kuna watu wamekufa kwa ujinga na upuuzi wake.
 
Kwa nini serikali isianzishe kuwa na police wa patrol na magari yapo kibao tu maana tunataka kitengo cha usalama barabarani na nyinyi tuone kazi yenu hasa sio mpaka sisi tuwaambie,kuweni na askari wa kusimamisha watu endapo watakamatwa wamelewa au wanaendesha vibaya huo ni mwanzo wa kuiingizia mapato serikali na Kutunza usalama wa raia ni mawazo yangu binafsi maana tunaona nchi zingine wanavyoendelea kwa njia hii
 
Dereva wa lorry la mchanga ndio mwenye makosa. Sijui alikuwa anataka kupiga U-Turn

Mwenye lorry la mchanga bila shaka!

Mwenye lorry la mchanga ndiye mwenye makosa.
Ukiangalia mchoro vizuri dereva wa roli la mchanga alikuwa keshaomba kuingia kwa kuashiria na indicator, lakini always daladala huwa wana haraka na most likely hakupenda kumpa mwenzake njia na yule naye akakomaa...nidhamu barabarani ni kitu muhimu mno
 
Kwani akiomba kuingia upande wa pili sikukubariwa au kukataliwa huyu anaonekana kafosi kuingia bila kutafakari anaebishananae anaabiria yeye ana mchana.siwapendi watu wanaobishana barabarani
 
Kwani akiomba kuingia upande wa pili sikukubariwa au kukataliwa huyu anaonekana kafosi kuingia bila kutafakari anaebishananae anaabiria yeye ana mchana.siwapendi watu wanaobishana barabarani
Hakuna watu wabishi kama madereva wa daladala huwa hawaombwi wakakubali, ila wao wakiomba ukubali, ukatae wanaingia....madereva wa daladala ni jipu.
 
Dereva wa lori la mchanga ana makosa maana alitaka kuingia kulia bila kuangalia aliemfuata nyuma yuko umbali gani kutoka kwake.

Kwa upande mwingine HEKIMA ingemtawala mwenye daladala kutoa nafasi ya mwenzake kuingia maana alikua amewasha indicator ya kuingia kulia ila kwa sababu ya haraka zake na roho mbaya yake akataka ambanie
 
Nafasi iliyopo kati ya lori la mchanga na daladala ni ndogo sana hata kama ameomba ku switch lanes
Kwa kiburi cha madereva wote kuonyesha nani mjanja nadhani wa DCM akaongeza speed na wa lori akaamua kuingia kwa nguvu ,matokeo yake ndio hayo kuua watu kizembe

Hivi huyo dereva wa lori la mchanga baada ya kuomba kuswitch lane alipokataliwa kwani angendelea kwenye lane yake kulikua na tatizo gani ?? Ama wa DCM kupunguza speed kumruhusu wa lori la mchanga ?
 
Ukiangalia mchoro vizuri dereva wa roli la mchanga alikuwa keshaomba kuingia kwa kuashiria na indicator, lakini always daladala huwa wana haraka na most likely hakupenda kumpa mwenzake njia na yule naye akakomaa...nidhamu barabarani ni kitu muhimu mno
Kuwasha indicator sio ruhusa ya kupita. Hujui mwenzio ana mwendo gani au anafikiria nini kichwani.
 
Laity daladala angemruhusu yasingetokea hayo .
Unajuaje labda mwenye lori kaingia ghafla na mwenye daladala kakosa hata nafasi ya kujitetea? Wenye dakadala wana fujo sana ila wako makini sana mara chache utakuta wamekwangua gari ya mtu pamoja na kuchomeka siku nzima
 
Kwa upande mwingine HEKIMA ingemtawala mwenye daladala kutoa nafasi ya mwenzake kuingia maana alikua amewasha indicator ya kuingia kulia ila kwa sababu ya haraka zake na roho mbaya yake akataka ambanie
mkuu hatujui mwendo wa hayo magari mawili pia inawezekana mwenye lori hakuiona daladala kabisa ndio akaingia, wenye mabasi kwa malori wana adabu sana.
 
Inawezekana pia DCM haikuwa na breki au ni roho mbaya na upumbavu wa madereva wa Daladala.
 
Back
Top Bottom