Ajali ya basi yaua watu 24 yajeruhi 56 | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Ajali ya basi yaua watu 24 yajeruhi 56

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Mar 2, 2010.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Mar 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  WATU 24 wamekufa papo hapo na wengine 56 wamejeruhiwa katika ajali ya basi la AM iliyotokea jana jioni eneo la mpaka kati ya Nzega na Igunga mkoani Tabora.

  Ajali hiyo imetokea majira ya saa 10: 15 jioni katika vijiji vya Kitangili na Migua baada ya basi aina ya Scania lililokuwa likitoka Arusha kwenda Mwanza kupinduka.

  Waliokufa ni wanaume 14, wanawake sita na watoto wanne huku majeruhi ni wanaume 35, wanawake kumi na watoto 7 majeruhi wanne wamepelekwa katika Hospitali ya Bugando mkoani Mwanza kwa matibabu zaidi.

  Mganga wa wilaya ya Nzega, Dk John Mwombeki alisema maiti pamoja na majeruhi hao wapo katika hospitali ya Nzega.
   
 2. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #2
  Mar 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  Naskia Kamanda wa Tabora, ACP Liberatus Barlow amesema jana kuwa mwendo kasi ndiyo uliosababisha kupinduka kwa basi hilo.hii njia nayo miaka hii inamaliza watu sana hasa eneo hilo la mpakani maeneo ya nzega sijui tatizo ni nini hivi hakuna matrafki?
   
 3. Tiba

  Tiba JF-Expert Member

  #3
  Mar 2, 2010
  Joined: Jul 15, 2008
  Messages: 4,515
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 160
  Wakuu,

  Hizi ajali ni za kujitakia. Zinaweza kuzuilika watendaji wetu serikalini wakiamua. Ukiangalia kwa hesabu za haraka haraka hilo basi lilikuwa limebeba zaidi ya abiria 80 wakati uwezo wake hauapashwi kuwa zaidi ya abiria 60.

  Je ni kwa nini askari wa usalama barabarani wanaruhusu magari ya safari ndefu kubeba abiria zaidi ya idadi inayokubalika?

  Kamanda Mwema upo hapo. You need to act before any more tragedy is added to the list.

  Tiba
   
 4. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #4
  Mar 2, 2010
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 135
  katika hali ya kushangaza, na kama ilivyo kawaida kwa Mji wa Nzega umeme hukatika takiribani mara 12 kwa siku. Hii ilitokea jana wakati majeruhi wa ajali hii walipofikishwa katika Hospitali ya wilaya ya Nzega wakihitaji huduma zinazotumia nishati ya Umeme . Huwezi amini Hospital ya Wilaya haina Generator! hivyo majeruhi walilazimika kupumzika gizani wakisubiri umeme urejee ili wapate huduma kama za ushonaji na X-rays.
  Ni vema tukafikia hatua ya kila hospital ya wilaya kuwa na nishati ya umeme mbadala.
  Inasadikiwa kuwa chanzo cha ajali hiyo ni mwendo wa kasi uliochangia kushindwa kuhimili kusimamisha basi hilo punde tairi lilipopasuka.
   
 5. Prisoner

  Prisoner Senior Member

  #5
  Mar 2, 2010
  Joined: Jan 26, 2010
  Messages: 120
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
   
 6. Mess

  Mess JF-Expert Member

  #6
  Mar 2, 2010
  Joined: Mar 2, 2009
  Messages: 667
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Lakini watanzania tufikie mahali angalau tuwe tunajali afya na vitu ambavyo vina risk kwa maisha yetu. Nimesafiri sana na mabasi na gari binafsi na gari za kazini. Wakati nikiwa kwenye mabasi mara nyingi huwa ni mlalamishi mara dereva anapokuwa na mwendo ambao naona si mzuri na wakati mwingine napata support kwa abiria wenzangu na wakati mwingine abiria huwa wananigeuka na kusema dereva endelea bwana, watu wengine hawajazoea kupanda mabasi (waoga) tena ni nakumbuka siku hiyo ilikuwa (Hood) na mbele kidogo akakosea kuovertake mpaka watu wakastuka lakini hawakusema sana maana wakati namwambia dereva hawakusupport. Sasa tukianza kuhagangaika na system ambazo tuna hakika hazifanyi kazi kikamilifu tutumie method 'B' kwanza wakati method 'A' inafanyiwa kazi. Jumatatu iliyopita nilikuwa naenda Iringa na Land cruiser kikazi nilikuwa na wenzangu kwa speed ya 120km/h lakini mabasi yalikuwa yanatupita sasa waliopanda humo ndani wanaona haya mambo? maana jana ilikuwa zamu ya wenzetu waliokufa na kesho au leo ni zamu yetu hivyo tusisubiri Mwema a act au traffic watimize wajibu wao ila sisi tutimize wajibu wetu kwanza, maana ndio victims. Watu wawapigie kelele madereva wasisubiri traffic au mtu mwingine, ukimwambia dereva mkawa na nguvu hata ya watu wanne kwenye basi kumwambia dereva huwa wanasikia maana wanajua hawa jamaa wataniletea balaa.
   
 7. Rubi

  Rubi JF-Expert Member

  #7
  Mar 2, 2010
  Joined: Oct 5, 2009
  Messages: 1,623
  Likes Received: 49
  Trophy Points: 145
  jamani ajali zimezidi siku hizi ukipanda chombo cha usafiri kufika na majaliwa la muhimu tumtangule Mungu kwa kila jambo.
   
 8. Regia Mtema

  Regia Mtema R I P

  #8
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 21, 2009
  Messages: 2,974
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 0
  Ooh jamani.
   
 9. cheusimangala

  cheusimangala JF-Expert Member

  #9
  Mar 2, 2010
  Joined: Feb 27, 2010
  Messages: 2,590
  Likes Received: 12
  Trophy Points: 0
  jamani kila cku tunasikia ajali ajali zitapungua lini!
   
 10. Azikiwe

  Azikiwe Senior Member

  #10
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 13, 2009
  Messages: 191
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Matairi ki-China?
   
 11. Lady N

  Lady N JF-Expert Member

  #11
  Mar 2, 2010
  Joined: Nov 1, 2009
  Messages: 1,919
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 135
  yawezekana
   
 12. Papa Mopao

  Papa Mopao JF-Expert Member

  #12
  Mar 6, 2010
  Joined: Oct 7, 2009
  Messages: 3,398
  Likes Received: 419
  Trophy Points: 180
  Kuna siku nilipanda basi linalojulikana kwa rangi nyekundu,basi hilo safari zake lilikuwa Dar Tunduma,aroooo!!! sitasahau njia nzima sikusinzia maana kona nilizoshuhudia pale kabla ya Kitonga mwe kidogo tupate ajali na siyo pale tu na hata karibia na Ilula na Iringa huko baadhi ya maeneo na Mbeya,dereva alikuwa high speed mpaka unashikilia kiti jamani khaaa!
  Sijui wanatafuta wale watu???
  Roho ilitulia niliposhuka pale Soweto Mbeya.
   
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
 1. This site uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
  By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.
  Dismiss Notice
Loading...