AJali nyingine yatokea mda huu Chalinze:


Kama wote tungefikiri namna hii, hata hizo ajali zingepungua. Lakini inapotokea gari imeshikwa na mtu anayefikiri mambo ya mwisho wa mwaka na uhusiano wa "kishirikina" hapo ajali itakua karibu sana.
 
Kikubwa si umeelewa,unadhani wote ni fundi magari kama wewe ayajue majina ya magari?Au ndo bange za mchana?

Kama hujui kitu bora usiwe unakurupuka ku post hapa as if unaogea nje..toyota ndogo ndo nini?au ndo magari yenu mnayotengeneza nyumbu? Kama sio fundi magari basi kaa report vitu vinavyohusiana na uvuvi wa samaki maana ndo fani yako
 

Umechanganya mkuu , madeva wengi wa route fupi za dar wanageuka ghafla kuwa madereva wa masafa marefu, anabeba family yake yote anawasha gari kuanza safari ya mbeya toka dar, amezoea kuendesha 12kms per day leo anageuka DEREVA wa 890kms, matokeo yake kufika Chalinze Tu anaanza kupambana na udingizi. Sasa mwisho wa mwaka na wakati wa sherehe kubwa madereva wa aina hiyo huwa wengi sana barabarani.
 
Last edited by a moderator:
Hvi mtu ukiyezoea kuendesha dar kila siku kwa mwaka mzima inakuwaje ushindwe kuendesha dar mbeya. Au unatakiwa ufanye mazoezi gani kabla ya safari?
 
Mi ntatoka ndani tarehe 1 january

Mkuu umenichekesha sana! Nakumbuka shekhe Yahaya aliwahi kumtabiria mtu mmoja (kwa kusoma kiganja cha mkono) kwamba atakufa kwa ajali ya gari ndani ya miezi 6. Huyu mtu akaamua hatatoka ndani kabisa kwa miezi hiyo sita. Alikuwa na hoteli na matokeo yake ni kwamba biashara yake iliyumba vibaya! Watu walipojua hawezi kutoka ndani wakachukua fursa. Lol.
 
poleni majeruhi wote mungu awatie nguvu
 
Last edited by a moderator:

Madereva wetu hawapumziki katika kipindi hiki. Wengi wanasinzia huku wakiendesha. Ndiyo maana utasikia akimwambia konda, nipigishe basi stori.

Siku si nyingi nilitoka ubungo around sa 5 (kutokana na ukaguzi wa sumatra) tulifika mwisho wa safari yetu saa nane usiku! Huwezi amini, dereva alisikika akisema 'NGOJA NIWAHI KULALA, KESHO NALIANZISHA TENA'.

Dereva wa aina hii, uendeshaji wake utakuwa salama siku inayofuata?
 
Mwendo kasi utaendelea kuleta madhara makubwa, poleni wote!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…