Ajali mbaya ya treni yatokea Ujerumani; watu wamepoteza maisha na wengi kujeruhiwa

beth

JF-Expert Member
Aug 19, 2012
3,879
6,356
germany2_3570803b.jpg

Watu 10 wamethibitishwa kufariki na wengine takribani 50 wamejeruhiwa baada ya treni mbili za kubeba abiria kugongana katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani.

Ajali hiyo imetokea katika mji wa Bad Aibling, takriban kilomita 60 kusini mashariki mwa mji wa Munich.

Polisi wa Bavaria wameandika kwenye Twitter kwamba watu wanane wamefariki, watu zaidi ya 50 wakaumia vibaya na takriban watu 100 wana majeraha madogo.

Moja ya treni hizo ilitka kwenye reli baada ya ajali hiyo na mabehewa yake yakabingiria, vyombo vya habari nchini Ujerumani vinasema.

Inaaminika magarimoshi hayo yaligongana ana kwa ana.

Maafisa wa kutoa huduma za dharura wamefika eneo la ajalii na helikopta zinatumiwa katika uokoaji.

Barabara zilizo karibu na eneo hilo zimefungwa, sawa na njia ya reli kati ya miji ya Holzkirchen na Rosenheim.
===================
Watu wanane wafariki ajali ya treni Ujerumani
Watu wanane wamethibitishwa kufariki na wengine wengi kujeruhiwa baada ya treni mbili za kubeba abiria kugongana katika jimbo la Bavaria nchini Ujerumani.

Ajali hiyo imetokea katika mji wa Bad Aibling, takriban kilomita 60 kusini mashariki mwa mji wa Munich.
Polisi wa Bavaria wameandika kwenye Twitter kwamba watu wanane wamefariki, watu zaidi ya 50 wakaumia vibaya na takriban watu 100 wana majeraha madogo.

Moja ya treni hizo ilitka kwenye reli baada ya ajali hiyo na mabehewa yake yakabingiria, vyombo vya habari nchini Ujerumani vinasema.

160209084827_bavaria_crash_640x360_reuters_nocredit.jpg

Maafisa wengi wa huduma za dharura wametumwa eneo hilo
Inaaminika magari moshi hayo yaligongana ana kwa ana.
Maafisa wa kutoa huduma za dharura wamefika eneo la ajalii na helikopta zinatumiwa katika uokoaji.
Barabara zilizo karibu na eneo hilo zimefungwa, sawa na njia ya reli kati ya miji ya Holzkirchen na Rosenheim.

At least 10 people have died and scores have been injured – 50 seriously – after two commuter trains collided in southern Germany, police have said.

The crash happened near the Bavarian town of Bad Aibling at 6.48am on Tuesday. Several carriages overturned after the trains, which were travelling in opposite directions, collided head on.

Police said the death toll had risen to 10, with 50 severely injured and a further 100 carrying light injuries.

Source: The Guardian
 
Treni mbili za abiria zimegongana uso kwa uso.. na kusababisha vifo vingi. Treni hizi zilikuwa katika njia moja,jambo ambalo limewashangaza wengi.
Ajali hii imetokea katika jimbo la Bavaria.kwenye mji mdogo wa Bad Aibling.Shughuli za uokozi zinaendelea.
_88177085_031359481.jpg

_88174951_031358491.jpg

_88178429_031359764.jpg
_88175531_031358743.jpg

Muda si mrefu uliopita treni mbili za abiria zimegongana na kusababisha vifo vingi. Treni hizi zilikuwa katika njia moja,jambo ambalo limewashangaza wengi.
Ajali hii imetokea katika jimbo la Bavaria.kwenye mji mdogo wa Bad Aibling.Shughuli za uokozi zinaendelea.
_88177085_031359481.jpg

_88174951_031358491.jpg

_88178429_031359764.jpg
_88175531_031358743.jpg

jamen usikute hawa wabaguzi wamewaua wahamiaji makusudi maana Bavaria ndo wanakoingilia ujerumani,,kama sio walale salama
 
jamen usikute hawa wabaguzi wamewaua wahamiaji makusudi maana Bavaria ndo wanakoingilia ujerumani,,kama sio walale salama
Hapana sio hujuma. Hizi treni zilipangiwa njia moja kimakosa.Zikakutana uso kwa uso . Opereta wa njia hii anahojiwa..kwanini kaziweka treni mbili katika njia moja.
 
Pole sana kwa maajeruhi na waliokufa wapate pumziko LA milele
 
human error
Yaweza kuwa ''human error'' au ''system malfunction'' hususan kwenye''signal system''..uchunguzi bado unaendelea.
Lakini huko Bavaria watu wanapiga bia balaa.Labda kuna mtu kaamka nazo...kasababisha ajali.
images
 
The reason for that accident really shocked me,both train drivers didn't have the timetable. How possible is this?
 
Nimejaribu kuwaza ingekuwa bongo, tungekuwa tunazungumzia vifo 500+ na sababu kubwa ni idadi ya watu ndani ya treni.

Hao jamaa unaweza kuta kwenye behewa ya watu 250 kuna watu kumi, ila bongo behewa ya watu 250 kuna watu 500.
 
Back
Top Bottom