Mi nipo eneo la tukio basi lililopata ajali ni NBS kutoka Tabora Kwenda Arusha na hadi sasa maiti ni SabaMungu aziweke roho za marehemu wote mahali pema peponi.....AMEN; Majeruhi wote MUNGU awape uhai wapone haraka"
Samahani kuna jamaa katinga na thread hapa naye anasema basi la Mohamed Trans litokalo Mwz~Dar limepata ajali hapo Igunga na muda ni huo huo sasa ni kwamba kuna ajali mbili tofauti maeneo hayo au?
Mi nipo eneo la tukio basi lililopata ajali ni NBS kutoka Tabora Kwenda Arusha na hadi sasa maiti ni Saba
Leo majira ya saa 4.00 asbh kumetokea ajali mbaya ya basi la NBS linalotokea Tabora kwenda Arusha, basi hilo lilipasuka Taili la mbele na kugonga mti na kuung'oa na kisha kupinduka, hadi sasa kuna maiti sita zilizowasilishwa Mortuari na Dereve wa gari hilo pia ni marehemu ila bado maiti yake haijatolewa kwani amebanwa hadi basi hilo likatwe ndiyo atolewe