Ajali mbaya maeneo ya makongo asubuhi ya leo

Ajali mbaya maeneo ya makongo asubuhi ya leo

JAFE

Senior Member
Joined
Sep 1, 2012
Posts
191
Reaction score
42
[FONT=Georgia, Times New Roman, serif] Hii ni ajali iliyotokea eneo la makongo ambapo gari ndogo imeangukiwa na gari la mchanga asubuhi hii. Juhudi za uokoaji za askari we jeshi la wananchi wakisaidiana na kikosi cha zimamoto na uokoaji walifanikiwa kumtoa dereva wa gari dogo mida ya saa 1:20 za asubuhi baada ya kukaa humo tangu saa 11 asubuhi. Gari aina ya Landrover maalumu kwa ajili ya kutoa misaada ya magari yaliyopata hitilafu barabarani likijaribu kutoa msaada.[/FONT]
[FONT=Georgia, Times New Roman, serif] Gari ambalo limeangukiwa na kufukiwa na mchanga uliokuwemo kwenye gari lililopata ajali. Dereva wa gari dogo bado yumo ndani.
[/FONT]

[FONT=Georgia, Times New Roman, serif] Gari ambalo limeangukiwa na kufukiwa na mchanga uliokuwemo kwenye gari lililopata ajali. Dereva wa gari dogo bado yumo ndani.
[/FONT]

[FONT=Georgia, Times New Roman, serif] Askari wa jeshi la wananchi wakijitahidi kutoa msaada wa kumnasua dereva aliyefukiwa ndani ya gari..

CHANZO: MATUKIO TZ BLOG
[/FONT]

[FONT=Georgia, Times New Roman, serif][/FONT]
 
Tragic.... Vipi dereva amenusurika mkuu?
 
Tatizo haya malori ni machakavu sana. Yanaletwa nchini kama damponi tu. Yanaendeshwa na wahuni wavuta bangi.
 
Nchi hii ya ajabu. Hayo ma-breakdown nayo ni machakavu kupindukia. Leo pale karihu na dstv, ali hassan mwinyi road nimekuta likivutwa na lori. Mengi ni ya mapolisi ndo maana hayakaguliwi wala hayaguswi.
 
Pongezi kwa jeshi la wananchi wa Tanzania wa pale lugalo. wamefanya juhudi kubwa kuhakikisha dereva wa gari dogo anatoka akiwa hai. Hilo limewezekana kijana ametolewa mzima akiwa hai na viungo vyote. Ilikuwa msisimko wa aina yake kwa waliokuwa kwenye tukio. Mungu apewe sifa kwa kumuokoa huyo kaka ni muujiza umetokea leo.
 
duh pole yake dereva huyu,nashukuru kusikia yuko salama....mimi formula yangu kuhusu malori ni either nalipita haraka au naliacha mbali....sikai nalo side by side kwenye foleni,naliacha mbali sana.
 
Pongezi kwa jeshi la wananchi wa Tanzania wa pale lugalo. wamefanya juhudi kubwa kuhakikisha dereva wa gari dogo anatoka akiwa hai. Hilo limewezekana kijana ametolewa mzima akiwa hai na viungo vyote. Ilikuwa msisimko wa aina yake kwa waliokuwa kwenye tukio. Mungu apewe sifa kwa kumuokoa huyo kaka ni muujiza umetokea leo.

Well.. what a happy ending 🙂
 
Dereva kaumia kidole tu
 
Attachments

  • 1397584158418.jpg
    1397584158418.jpg
    52.9 KB · Views: 226
Back
Top Bottom