BIGURUBE
JF-Expert Member
- Mar 11, 2014
- 6,748
- 4,257
Kuna taarifa nimezipata kuna mabasi matano yaliyokuwa yakitokea Arusha yamegongana...mwenye habari kamili tunaomba updates
JAMIIFORUMS: Habari hii si ya kweli, ni ajali ya 2012 na ilihusisha mabasi ya simba mtoto na Dar express pia ilishawahi kuzushwa tena Septemba 2014
CHANZO: Mwananchi(Septemba 10, 2014)
JAMIIFORUMS: Habari hii si ya kweli, ni ajali ya 2012 na ilihusisha mabasi ya simba mtoto na Dar express pia ilishawahi kuzushwa tena Septemba 2014
Uongozi wa Kampuni za Mabasi ya Dar Express na Simba Mtoto umefafanua kuwa hakuna ajali iliyotokea kama ilivyoripotiwa jana.
Hatua hiyo imekuja baada ya kuwapo taarifa za ajali eneo la Wami, Darajani ambazo zilidaiwa kuhusisha mabasi ya Dar Express na Simba Mtoto.
Ajali ya mabasi hayo iliwahi kutokea eneo hilo mwaka 2012, lakini si juzi kama ilivyoripotiwa.
Msemaji wa Polisi mkoa wa Pwani, Hassan Juma alisema juzi kuwa walipata taarifa za ajali na walikuwa wanakusanya taarifa zaidi.
Alipoulizwa Kamanda Msaidizi wa Polisi Mkoa wa Pwani, Athumani Mwambalaswa jana asubuhi, alisema kuwa ofisi yake haina kumbukumbu za kutokea ajali kama hiyo.
Alipotafutwa Kamanda wa Polisi mkoa wa Tanga, Frassier Kashai jana, naye alisema kuwa hakuna kitu kama hicho.
Pamoja na kuwapo taarifa hizo, tumethibitisha pasi na shaka kuwa hazina ukweli. Tunaomba radhi kwa wote walioguswa au kupata usumbufu wa taarifa hiyo ambayo tuliichapisha jana katika gazeti hili-Mhariri.
CHANZO: Mwananchi(Septemba 10, 2014)