Ajali kimara Korogwe

Ajali kimara Korogwe

mkonowapaka

JF-Expert Member
Joined
Feb 19, 2010
Posts
1,492
Reaction score
771
Source clouds fm
Lori lililobeba ng'ombe likitokea morogoro kuelekea dsm limegongana na basi la abiria na kusababisha vifo vya watu. 10. Hapo hapo....tupeni updates mliopo eneo la tukio
 
duh...hawa watu wanapanga kutuua nini? Kila siku jamani tunakufa tu
 
Du mbaya sana,Mungu awalaze marehemu wote mahali pema,
 
......Ohhhh!! Ajali tena. Mungu awarehemu marehemu.
 
Ni kweli imetokea. Source: Mwananchi
 
Mwananchi Communications Ltd Kuna Ajali mbaya Imetokea maeneo ya
Kimara resort tunaendelea kupata
taarifa then tutakujulisheni , ila kwa
ufupi magari manne yamegongana na
watu wameumia vibaya sana na kuna
uwezekano wapo Wengi waliopoteza maisha
 
Ooh ajali zinakua issue hasa mwishoni mwa mwaka hakika madereva tuwe makini tutamalizana hivi hivi
 
Source clouds fm
Lori lililobeba ng'ombe likitokea morogoro kuelekea dsm limegongana na basi la abiria na kusababisha vifo vya watu. 10. Hapo hapo....tupeni updates mliopo eneo la tukio
Kweli leo siku ya shetani, mimi nasafiri toka Iringa tangu saa2 na nusu asubuhi, mpaka mda huu tuko hapa kimara suka kuna foleni ya hatari. Pamoja na hayo kulikuwa na ajari Chalinze ambapo malori mawili yaligongana na kusababisha msongamano tulikaa hapo kwa zaidi ya saa moja, kitonga pia tumekuta malori mawili yakiwa yamegongana na moja likiwa linaning'inia kutaka kuangukia katika cliff. Jamani tuombeni mwezi Dec mgumu sana Tanzania hasa kwa matukio ya ajali.
 
Lakini simliambiwa na Mwaintelejensia Mwema kuwa kutakuwa na ajali lakini hamkusikia sasa mmeona limewakuta
 
poleni wahanga.
inabidi madereva sasa wapitie chuo cha usafirishaji itasaidia kupunguza ajali
 
Wadau kuna roli lililokuwa linatokea ubungo nimehama njia maeneo ya kimara resolt na kugongana na coaster na kuua mtu mmoja kwenye bus lakini kwa bahati mbaya wapita njia nane nao wamepoteza maisha ila hali sio nzuri kwa sababu watu ni wengi sana kiasi cha kusababisha msongamano wa magari mengi sana yaendayo ubungo pia yanayotoka ubungo pia fujo zimeanza kiasi cha wengine kupigana hapa!na tukumbuke sehemu hii ndio iliyoua watu pia kwa kudondoka kwa container
Wadau naomba kuwasilisha!
 
Source clouds fm
Lori lililobeba ng'ombe likitokea morogoro kuelekea dsm limegongana na basi la abiria na kusababisha vifo vya watu. 10. Hapo hapo....tupeni updates mliopo eneo la tukio

ng'ombe nao wamenusurika?
Masikini kitoweo...
 
Back
Top Bottom