Ngaliba Dume
JF-Expert Member
- Oct 6, 2010
- 1,710
- 3,675
Kuna ajali mbaya sana imetokea maeneo ya Mbezi kwa Msuguli jioni hii mkabala na maegesho ya malori ya kutoka mikoani.Ajali imehusisha gari (daladala) inayofanya safari zake kati ya Mbezi Mwisho na Muhimbili.
Ajali imeuwa watu wawili katika eneo la tukio na kuacha wengine wajeruhi.Waliofariki na mtoto mdogo (wa shule) ambaye amepasuliwa kichwa na ubongo kumwagika chini na mwanaume mmoja wa makamo.
Eneo limejaa damu na kutapakaa ubongo wa binadamu.Ni ajali ambayo huwezi kutamani kutazama picha wala kuziangalia maiti.Ajali imesababisha foleni ya zaidi ya saa moja na nusu.
Chanzo cha ajali ni gari ku-fail kushika breki na kusababisha kupitia waenda kwa miguu waliokuwa wanavuka kwenye kivuko-milia eneo la Msuguri.Waliokuwa kandokando wamekoswakoswa na gari kuangukia mtaroni.
Askari wa Usalama barabarani maarufu kwa jina la Mashaka (wanaopita njia ya Morogoro wanampata) ambaye karibu kutwa ya leo amepita vituo vyote kuwaondoa bodaboda na meza za wauza ndizi na kina mama wauza samaki,amenusurika kugongwa,askari wa kike naye amepoteza kiatu chake baada ya kuruka mtaroni kukwepa kifo.
Isingelikuwa oparesheni iliyoongozwa na askari wa barabarani kuwaondoa bodaboda na wauza baishara kando ya vituo vya daladala,leo Msuguri kungegeuka "machinjio" na msiba mkubwa.
Walio na ndugu maeneo ya Msuguri,au mtoto wa kike ambaye mpaka sasa hajafika nyumbani,wafuatilie polisi kujua maiti zilipopelekwa na kwenda kutambua miili ya marehemu.
Tuombe Mungu kuzikwepa roho za mauti na ajali zenye uzembe,madereva watazame vyombo vya moto kabla ya kuingia barabarani.Waendesha bodaboda waepuke kuegesha kando mwa vituo vya daladala na kuongeza msongamano unaosababisha ufinyu wa maegesho,na wale wauza pweza,karanga,ndizi,mahindi yenye mkolezo wa chumvi,matikiti na machungwa,wasogeze meza zao ili kutanua eneo la maegesho ktk vituo vya daladala