beth
JF-Expert Member
- Aug 19, 2012
- 3,879
- 6,356
Watu wanne wamefariki dunia katika ajali baada ya basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kwenda jijini Mwanza kugongana na gari dogo katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga
Ajali hiyo imetokea jana jioni ambapo mashuhuda wa tukio hilo wamedai kuwa ilisababishwa na gari ndogo iliyokuwa katika mwendo kasi ambayo ilipoteza uelekeo na kisha kuligonga basi hilo.Watu wawili waliokuwa katika gari hilo akiwemo dereva walifariki dunia papo hapo
Mganga mfawidhi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Shinyanga Dkt Albert George Masigati amesema kati ya saa 12 na saa moja usiku wa kuamkia leo walipokea miili ya marehemu wanne katika hospitali hiyo ,wote wakiwa ni wanaume na majeruhi wanane,kati yao wanawake wanne na wanaume wanne.
Hata hivyo Dkt Masigati amesema huenda idadi ya majeruhi ikaongezeka kutokana na taarifa kuwa baada ya ajali hiyo kutokea baadhi ya majeruhi walikimbizwa katika hospitali ya Kolandoto na Kishapu.
Dkt Masigati amesema hakuna majeruhi aliye katika hali mbaya na kwamba bado wanaendelea kuwafanyia uchunguzi .