Ajali: Basi la Luwinzo, Dar-Njombe lagonga lori na kusababisha vifo

Maboso

JF-Expert Member
Feb 18, 2013
5,164
5,762
Basi la abiria la kampuni ya Luwinzo linalofanya safari za Dar es salaam - Njombe limepata ajali asubuhi hii likitokea Njombe kuelekea Dar. Inasadikika limeua baadhi ya abiria na majeruhi ni wengi. Ajali imetokea maeneo ya Kinegembasi Kata ya Mbalamaziwa (Mufindi).

====
Hadi sasa, waliothibitika kupoteza maisha ni wawili na Wengine 21 kujeruhiwa.

ajali_luwinzo2.jpg

ajali_luwinzo1.jpg

ajali_luwinzo3.jpg
 
Last edited by a moderator:
hii tabia ya madereva kuzoea barabara inatucost sana wasafiri..napendekeza wawe wanabadilishiwa route kila baada ya muda.
 
Huu ni upuuzi wa dereva lazima aliovertake akaona kuna gari inakuja akarudi akaingia kwenye lori. Ila ajali nyingi zinazotokea Iringa zinasababishwa na Police. Torch ni nyingi sana sasa madereva wanapofika sememu ambazo hazina tocho wanalazimika kukimbia sanaaaa ili kufidia mda uliopotea sehem zenye torch. Namna pekee ya kupunguza ajali ni kutumia ratiba tu.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
 
Ratiba hiyohiyo wanakimbia sana na wanapokaribia kituo fulani kama wako mbele ya muda basi watawachimbisha dawa kwa lazima hata kama ni dakika 45
 
Poleni majeruhi dah! Kuna mtu humu roho inamuuma vibaya mno maana yeye ndie anapenda awe wa kwanza kuleta habari za ajali.
 
Huu ni upuuzi wa dereva lazima aliovertake akaona kuna gari inakuja akarudi akaingia kwenye lori. Ila ajali nyingi zinazotokea Iringa zinasababishwa na Police. Torch ni nyingi sana sasa madereva wanapofika sememu ambazo hazina tocho wanalazimika kukimbia sanaaaa ili kufidia mda uliopotea sehem zenye torch. Namna pekee ya kupunguza ajali ni kutumia ratiba tu.

Sent from my BlackBerry 9320 using JamiiForums
Mimi nadhani suala la torch si kigezo cha kumfanya mtu akimbize gari, kikubwa ni kuheshimu sheria na alama za usalama barabarani. Hakuna haja ya kulazimishana kufuata sheria, tujenge mazoea ya kutii sheria bila shuruti.
 
Dah!poleni sana ndugu zetu ni masikitiko makubwa sana.Nipo Congo lkn habari za homu ni lazima nizipitie kila wakati.
 
Hili jipu la ajali za barabarani limekosa mtumbuaji. Kama taifa inaonekana tumeshindwa kutafuta ufumbuzi. Tochi zipo, askari wapo, ajali kama kawa.
 
Mbaya sana, nina rafiki yangu alikuwepo humo ni mmoja wa majeruhi amevunjika mguu, na alikuwa anakuja arusha kwenye mahali.....Mungu awaponye majeruhi wote!
 
Back
Top Bottom