Ajali barabarani chanzo ni rushwa NTI

nndondo

JF-Expert Member
Feb 1, 2010
1,251
895
Walimu wa chuo cha usafirishaji Ubungo wamebobea kwa rushwa ndio haswa chanzo cha ajali za ajabu ajabu kama hii ya City Boys. Ndugu zangu kwa sasa chuo hiki kimepokea wanafunzi wa mafunzo mbalimbali ya udereva wasiopungua 167, mafunzo haya yalianza July 1 na yataisha julai 18. Wanafunzi wamekua na mafunzo ya darasani kwa wiki moja na wiki ijayo wataanza mafunzo kwa vitendo. Cha kushangazi ni pale ambapo siku ya jana walimu wote walioingia darasani walikua wanachimba mkwala mzito kuwa si kila mwanafunzi aliyepo hapo atapata cheti.

Mwenyekiti wa darasa apewa maelekezo
Ni jambo la kushangaza sana na la aibu pale Mwenyekiti wa darasa alipopewa maelekezo ya kuchukua majina ya watu wanaotaka kupata cheti na yeye kufanya hivyo. Majina ya watu kadhaa yalichukuliwa dhidi ya malipo ya T.shs 35,000/- kwa kila jina. Mwenyekiti alituhakikishia kuwa mara tu tutakapopatiwa namba za mitihani, namba hizo zitawakilishwa kwa hao walimu walioelekeza hivyo ili kuhakikisha kwamba wahusika wanapasi na kupewa vyeti. Hili jambo sio majungu ni jambo la wazi kabisa limefanyika jana na watu wameandika majina na kutoa pesa hizo kwa Mwenyekiti.

Mafunzo haya ni wizi wa fedha zetu walimu hawa wafukuzwe kazi mara moja
Hii inamaana hakuna tena faida ya kusoma wala kufanya mitihani kwa maana hao waliollipa hela bila kujali uwezo wao au ufaulu wao wanaenda kupewa cheti. Jambo la pili, hili swala limetukatisha tamaa sana sisi ambao tunauwezo wa kufaulu na tunauzoefu wa kuendesha, na sio sisi tumegoma kutoa tena hela wakati tayari tulishalipa 200,000/- za mafunzo haya na vyeti.

Mkuu wa Chuo na Afanda Mkinga, TAKUKURU ingilieni swala hili mara moja
Tunaomba TAKUKURU na askari wa Afanda Mkinga waingilie swala hili mara moja maana wiki ijayo ndio ya mwisho kwa kozi hii, ushahidi uko wazi, ni pm kwa majina ya waliolipa na huyo mwalimu anaye coordinate hilo zoezi, inaonekana liko institutionalised maana linafanyika wazi.

Chukua Hatua Nusuru maisha ya Watanzania
Tuko tayari kushirikiana na uongozi wowote utakaokua tayari kufuatilia rushwa hii iliyosababisha vifo vya watu kule Singida juzi juzi, tunaamini kabisa wale madereva wote wawili kama walisomea chuo hiki, watakua walipatiwa vyeti kwa rushwa ndio maana Jeshi la Polisi limebaini kuwa kulikua na uzembe katika uendeshaji. Tuko tayari kufanyakazi na gazeti la uchunguzi kama Jamhuri kubaini hasara taifa hili linayopata na vifo vinavyosababishwa na mambo haya ya rushwa. Chuo kimetukantisha tamaa sana na kimeshusha heshima yake tangu sasa. Mkuu wa chuo kama unasoma hapa ni pm nikupe details na hao waliotoa rushwa majina yao tunayo na tutafuatilia matokeo yao, kama kutakua na kuonewa watu wasiotoa rushwa tutafikisha swala hili Mahakamani, muda umefika wasiotaka kufanyakazi na wasile, tumechoshwa na rushwa, majipu lazima yatumbuliwe

Ni pm kwa taarifa zaidi na nataka kama chuo
 
Back
Top Bottom