Hebu fikiria umeamka asubuhi, kisha hakuna hata maji ya kuoga unaamua kwenda kuchota maji ya kisima karibu na home ili uoge fasta fasta uwahi kazini. Unafika kisimani unakuta kumbe mtoto katumbukia na kufa, utapiga simu polisi uwambie huku kumetokea ajali au kero?
Nahisi hujanielewa;
Fikiria umepiga shati lako jeupe na Tai moja matata sana kisha unaenda zako kwenye interview ya job ambayo unaipenda sana huku ukiwa ushapigika sana mtaani, ile unafika pundamilia ili uvuke barabara kunatokea gari linakwenda speed mbaya nawe unafanikiwa kuliona na kusimama ila jamaa mmoja anavuka kichwa kichwa, kisha gari linamgonga na damu inakurukia na kuchafua shati lako. Tukio lote kwa ujumla wewe utalichukulia kama ajali au kero?
Kweli we umemaliza form four mwaka huu, yani hujaelewa tu!!
Okay! Chukulia unapika ugali ile umeanza kuusonga tu, unagundua unga hautoshi hivyo unaamua kwenda dukani fasta kuongeza unga, ila karibu na kwenu kuna kijipori, na wakati unarudi toka dukani nyoka akakuuma, hiyo kwako itakuwa ajali au kero?