Aishi na Kisu Ndani ya Kichwa Chake Kwa Miaka Mitatu | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Aishi na Kisu Ndani ya Kichwa Chake Kwa Miaka Mitatu

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by MziziMkavu, Sep 28, 2010.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Sep 28, 2010
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,614
  Trophy Points: 280
  :lol:

  [​IMG]
  Edeilson Nasciento akiwa ameshikilia picha ya x-ray inayoonyesha kisu kilichokuwemo ndani ya kichwa chake
  Mwanaume mmoja wa nchini Brazili alilazimika kuishi miaka mitatu akiwa na kisu ndani ya kichwa chake ambacho alichomwa wakati ugomvi ulipozuka kwenye baa aliyokuwa akipata ulabu. Miaka mitatu iliyopita mziba viraka vya matairi ya gari wa nchini Brazili, Edeilson Nasciento mwenye umri wa miaka 29, alichomwa kisu kichwani wakati ugomvi ulipozuka kwenye baa aliyoenda kupata ulabu.

  Kisu hicho chenye urefu wa sentimita 10 kilizama ndani ya kichwa chake na kuhatarisha maisha yake.

  Kwa bahati mbaya, hospitali aliyowahishwa kwaajili ya matibabu walisema kuwa hawana uwezo wa kukitoa kisu hicho kwani kipo karibu sana na ubongo wake hivyo hatua yoyote ya kujaribu kukitoa kisu hicho kungeyatia maisha yake hatarini.

  Mpini wa kisu hicho uliojitokeza nje ya paji lake la uso ulikatwa lakini kipande kikubwa cha kisu hicho kiliachwa ndani ya kichwa chake.

  Nasciento alilazimika kuendelea na maisha yake ya kawaida akiwa na kisu ndani ya kichwa chake.

  Ikiwa ni miaka mitatu tangu tukio hilo lilipotokea mwaka 2007, wiki iliyopita maumivu makali ya kichwa yalimfanya Nasciento alazimike kukimbilia tena hospitali kukiondoa kisu hicho.

  Nasciento alifanyiwa operesheni kubwa iliyochukua masaa matatu kukiondoa kisu hicho ambacho kimekuwa ndani ya kichwa chake kwa miaka mitatu sasa.

  Akiongea baada ya kumalizika kwa operesheni hiyo Nasciento alisema "Hivi sasa najihisi vizuri zaidi".

  Nasciento anatajia kuruhusiwa kurudi nyumbani kwake wiki ijayo.
  chanzo: NIFAHAMISHE Tanzania news portal .: Habari za Tanzania :.
   
Loading...