Airtel yaweka mgomo baridi?

Rihana

JF-Expert Member
Apr 26, 2013
498
250
Toka jana vocha haziingii walituma ujumbe mfupi eti tuweke kwenye Airtel money...leo nimeingia Airtel money kununua salio inaniambia system is busy...sijaona tangazo lolote kwenye vyombo vya habari wakiomba radhi...hiki kiburi wanatoa wapi? Au ni njama ya kutaka wateja waingie kwenye huduma ya Airtel money ambayo imedorora??natamani nimtukane tusi la nguoni huyo MD wao mhindi ila Mod atanimaliza kwa kweli inakera sana PUM''BU!

Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
 
mbinu zao ili watu waingie airtel money,huu ubunifu wao naona wameungundua hv karibuni. mm nimehamia tigo baada ya kujaribu kuingiza vocha niunge internet yangu ikanigomea tokea jana.
 
nilihama tigo, nikahama voda kwa ajili ya use..nge huu, sirudi nilipotoka hapa ni kusonga mbele tu...ila sijui niende wapi?
 
Seriously! Kwa nini wamekaa kimya bila ya kujali madhala yaliyo wakumba wateja wao kwa kukosa mawasiliano, wanajifanyia wapendavyo bila ya kutoa taarifa mapema - zingekuwa ni nchi za wenzetu wangepashwa kutulipa fidia.
 
Toka jana vocha haziingii walituma ujumbe mfupi eti tuweke kwenye Airtel money...leo nimeingia Airtel money kununua salio inaniambia system is busy...sijaona tangazo lolote kwenye vyombo vya habari wakiomba radhi...hiki kiburi wanatoa wapi? Au ni njama ya kutaka wateja waingie kwenye huduma ya Airtel money ambayo imedorora??natamani nimtukane tusi la nguoni huyo MD wao mhindi ila Mod atanimaliza kwa kweli inakera sana PUM''BU! Sent from my BlackBerry 9900 using JamiiForums
Mwaka jana tulituma fedha via Airtel kwenda kwa jamaa zetu, fedha hazikuwafikia wahusika - tulipo kwenda kuchunguza ilionekana ni kosa lao, ilituchukuwa zaidi ya miezi sita kurudishiwa fedha zetu na hii na baada ya kuwatishia kuwafikisha mbele ya vyombo vya dola, naona bado wana mentality za mashirika ya UMMA -hawajali kitu.
 
Hamieni voda.......mcheke mitandao yote.....bhaaaaasi.......
 
Back
Top Bottom