Airtel wanakusanya pesa ya ist?!!

Airtel wanakusanya pesa ya ist?!!

nkyagila

Member
Joined
Sep 4, 2013
Posts
36
Reaction score
3
Nimesikitishwa sana na tabia ya hii ya airtel, naona wanatumia nguvu sana ya kuiba pesa za wateja wao kulipia hizo IST. Mie nina utaratibu wa kuweka kifurushi cha yatosha cha Tshs.10, 000/- kikiwa na gb 800 kwa ajili ya matumizi ya mwezi,hivyo niliweka kifurushi wiki jana lakini huduma ya internet ilikata ghafla kuangalia salio kifurushi cha internet kilikuwa kimeisha na kubaki muda wa maongezi peke yake, nikaona isiwe tabu nikaamua nijiunge na ile huduma nyingine sijui inaitwaje ila unapiga *148*88# nikanunua kifurushi cha mwezi cha Tshs.10, 000/- chenye
gb 3 hiyo ilikuwa tarehe 06.02.2015 'funny things' tarehe 07.02.2015 internet ikakata nikadhani labda sehemu niliyopo hakuna mtandao, likaja wazo la kuangalia salio kumbe wamekwishafanya mambo yao tena, kuwapigia huduma kwa wateja wakasema watalifanyia kazi na nitatumiwa msg baada ya nusu saa, nimesubiri hiyo meseji yao bila mafanikio, ndipo nilipoamua kuwapigia tena leo saa nane mchana wakasema niwapigie baada ya masaa 3 tatizo litakuwa liishashughulikiwa.Jambo la ajabu ni kuwa nimepiga simu hakuna response yoyote zaidi ya kuendelea kukata Tshs.60 kila ninavyopiga simu. Hiyo ni kwangu au? Nauliza tu. Mie mgeni humu jamvini.
 
Mimi pia wameniibia sana, huwa napata sms kuwa nimezawadiwa airtel money nikiangalia salio sioni chochote zaidi ya kukatwa salio lililopo tu!
 
Hata sijui tuhamie mtandao gani maanake yote ni mijizi tu
 
Back
Top Bottom