Airtel, Tatizo liko wapi?

Roadmap

JF-Expert Member
Aug 19, 2013
2,898
5,797
Hawa jamaa wakuitwa Airtel wapo kwenye Autopilot pengine chombo kishafeli na rubani wameshavaa Parachute au Life Jacket sisi abiria hatujui kinachoendelea.

Hawa Ndugu zangu licha ya kuwa na Coverage kubwa nchini ila kwa sasa kwa kweli huduma zao ni mbovu jana nimetuma message ikaonesha imefail ila ajabu niliyemtumia kaniambia hio message ameipata leo hii. Yaani sms itumwe jana then ifike leo tena mtumaji haimuoneshi delivery report!

Nafahamu Sector ya mawasiliano haina monopoly hivyo kung’ang’ana na provider mmoja ni kujichosha ila sasa utafanyaje na official number yako ni Airtel?

Kwa suala la internet huwa silalamiki maana nina simcard zote, net ya provider huyu ikiyumba natoa chip yake naweka kwa wallet naweka chip ya provider mwingine mpaka nisikie kajirekebisha .

Sasa ndugu zangu hawa Airtel hata ku provide tu basic services kama Kulipa umeme, Kupiga simu au kutuma text napo mnakwama hio kitengo cha ICT watu ni wamelala au?
 
Nakusapot kk...airtel sahv wanazingua kwa kwl, mm nilijiunganga kifurush cha internet kupitia airtel money, cha ajabu nikatumiwa message ya airtel money kwamba nimefanikiwa kujiunga, ila data za internet sikupata...

Nikawapigia nikaambiwa ni tatizo la kiufundi, baada ya siku 3 nitarudishiwa pesa yangu, tangu mwezi wa 6 mpaka sasa mwez wa 8 sijapewa hata sh 10...huu ni uhuni wa ajabu sana.
 
Unanunua luku token haiji.
 
Aisee pole mkuu hawa jamaa ni shida tupu
 
Airtel ni vilaza kwa sasa ,wana matatizo kibao unaweza ukampigia mtu wakakwambia hizo namba hazipo wakati siku zote unazitumia kuzipiga
 
lawama za nn!?, si muhame mtuachie mtandao wetu...
 
Pia kuna shida nyengine nimeiona siku mbili hizi,mtu unapiga simu inakaa kidogo kisha inakuja kiujumbe “CALL ENDED” unang'ang'ana kupiga kwa sababu ni urgently unataka kufahamu kuhusu jambo lako ila inajirudia rudia hivyo hivyo kumbe yule unayempigia kule anaona kama unam-beep,naye anakupigia mnakuwa sasa mnatafutana hewani,yule kule anajua umem-beep na wewe unadhani ni tatizo kidogo tu la mtandao.

Yupo mmoja akaniambia...sasa si ubip mara moja tu mara sita zote za nini?nilifedheheka sana ukichukulia ni mtu nilikuwa na miadi naye ya kibiashara unadhani nilionekanaje?Airtel mbadilike wateja tunadhalilika kwa makosa yenu ya kipumbavu!
 
Msicheze na kutoa gawiwo/dividend + ku-surrender shares zenu kwa wajomba huku hamjajipanga.

Lazima mtu ayumbe hapo.
 
kuna thread niliweka kuwalalamikia airtel kuhusu muamala niliofanya kufeli (hela kwangu imekatwa ila ninayemtumia hajapata) wakanijibu kua TATIZO LITAKUA LIMETATULIWA NDANI YA SAA 72 na wakaongeza kwa kusema kwao SIKU MOJA NI MASAA 8,,, nikawauliza kwahiyo hayo masaa 72 natakiwa kusubiri siku 9!? yule mdada akajibu NDIO TENA EXCLUDE WEEKENDS! nikakata simu nikanywa maji nikajichekea ihiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiiii.
 
Kwa kweli wamezidi wakati ulikuwa mtandao wa kistaarabu. nikituma sms unapata delivery report ya expired unarudia kutuma mara kadhaa text ile ile na report bado ni expired kumbe bana upande wa pili zinadeliver, mpokeaji anabaki tu kukushangaa. Airtel rekebisheni mitambo yenu!
 
Yule Muhindi alikuwa anamfurahisha JPM siku ile ikulu, ohoo tutatoa bilioni moja kila mwezi hiyo kabla ya gawio halali.

Sasa wafanyakazi nao wanataka nyongeza, si pesa ipo ya kugawa hovyo?!

Mwisho tutasikia wanafunga ofisi kwasababu ya kiherehere na kujipendekeza kusikokua na maana.
 
Na Airtel money warudisha gharama za kutuma pesa kwenda Airtel. Hilo ndilo moja wapo ya jambo pekee lililonibakisha Airtel. Sasa kwaherini
 
Yule Muhindi alikuwa anamfurahisha JPM siku ile ikulu, ohoo tutatoa bilioni moja kila mwezi hiyo kabla ya gawio halali.

Sasa wafanyakazi nao wanataka nyongeza, si pesa ipo ya kugawa hovyo?!

Mwisho tutasikia wanafunga ofisi kwasababu ya kiherehere na kujipendekeza kusikokua na maana.
B.1 kila mwezi mbali na gawio halali,huyu muhindi huyu
 
Nakusapot kk...airtel sahv wanazingua kwa kwl, mm nilijiunganga kifurush cha internet kupitia airtel money, cha ajabu nikatumiwa message ya airtel money kwamba nimefanikiwa kujiunga, ila data za internet sikupata...

Nikawapigia nikaambiwa ni tatizo la kiufundi, baada ya siku 3 nitarudishiwa pesa yangu, tangu mwezi wa 6 mpaka sasa mwez wa 8 sijapewa hata sh 10...huu ni uhuni wa ajabu sana.
Nmepata same case na pesa haijawahi kurudi!
 
Airtel saiv hawaeleweki niliamusha pesa zangu kidogo kutoka Airtel money kwenda kwenye TIMIZA AKIBA Yao imetokea nimekwama leo siku ya nne toka nimeahamisha hela kutoa kwenye TIMIZA kurudisha kwenye Airtel money niweze kutoa hela haitoki naambiwa tunashughulikia muamala wako.

Huduma kwa wateja majibu wanayotoa ndiyo yanazidi kukera zaidi ukiwabana kwa maswali wanakwambia ndani ya masaa 24 na kukata simu.

Msaada jamani mwenye uelewa kidogo kipi cha kufanya.
 
Airtel saiv hawaeleweki niliamusha pesa zangu kidogo kutoka Airtel money kwenda kwenye TIMIZA AKIBA Yao imetokea nimekwama leo siku ya nne toka nimeahamisha hela kutoa kwenye TIMIZA kurudisha kwenye Airtel money niweze kutoa hela haitoki naambiwa tunashughulikia muamala wako. Huduma kwa wateja majibu wanayotoa ndiyo yanazidi kukera zaidi ukiwabana kwa maswali wanakwambia ndani ya masaa 24 na kukata simu.
Msaada jamani mwenye uelewa kidogo kipi cha kufanya.
Pole sana mkuu!
 
Back
Top Bottom