Airtel Money

WIMICKY

JF-Expert Member
Joined
Jun 9, 2011
Posts
1,439
Reaction score
1,575
Habari Wakuu!! Jamani mimi ni Wakala wa hizi huduma za simu kama vile M-pesa/Tigo pesa ila hawa jamaa wa akatwi mtu nilikuwa sijawa na huduma zao ofisini kwangu. maana mwanzo nilituma fomu nawakaniletea Till ya jina la mtu mwingine wakati walipewa vitambulisho vyangu nikawaludishia line yao hivi majuzi wakaja ofisini kwangu nakunipa Till ikiwa ipo chini ya wakala mkuu walienae eneo letu kwa maeelezo baada ya muda si mrefu watazibadilisha majina kwa sababu wateja walishaanza kuniulizia ulizia nikaichukua baada ya hapo nikaanza kuifanyiakazi mwezi 1 nikapewa kamisheni huu wa pili wakaifunga kisa eti haijasajiriwa nikafuatilia wakasema imesariliwa ila wanataka log book kuhakiki kama nafanya kazi(nikawapa log book) nikawafuata tena wakaanza kutupiana mpira mara mfuate fulani ukifuata nae anasema sina uwezo wa kufungua kibaya zaidi kuna hela zangu nilizo kuwa nafanyia kazi (mpaka sasa wiki 3) kwa hiyo hawa jamaa hawajajipanga ki ukweli wanafanya kwa kubuni tu! mawakala wenzangu msithubutu kuacha hela nyingi kwenye Till za Airtel (kamazimo ziamisheni nakuziweka kwenye mitandao mingine)msijemkafanyiwa kama nilivyofanyiwa mpaka sasa sifahamu hizo hela zangu kama zitaludishwa au ndo wamechukua maana wanasema HAKATWI MTU!!!!!!!!
 
Binafsi nina uzoefu pia na hizi huduma za fedha za makampuni ya simu. Voda ndio wako organised kulinganisha na wengine. Airtel wanajaribu sana kuiga lakini bado kazi wanayo. Tatizo la Airtel ni kama wote unaowaona hawana uamuzi hata kama jambo ni dogo. Anapasia mpira kwa mwingine na mwingine anafanya hivyo hivyo. Nilishawahi kuweka fedha kwenye Airtel Money kisha kukawa na shida, nilifuatilia kwa mwezi mzima ikabidi niandike notisi ya kuwashitaki ndo fedha wakarudisha. Nilishangaa sana nikajiuliza vipi kama ni mtu wa kijijini anaweza kweli kufanya kama nilivyofanya? Kumbe wanaoliwa fedha yao kwa namna hiyo ni wengi.

Ushauri kuhusiana na tatizo lako ni kufuatilia kwa nguvu zote na ikibidi andika barua kabisa. Unajua ukiandika barua kama kuna tatizo lazima wakujibu officially. Ni njia ya kuwalazimisha wafanye kazi wanayotakiwa kufanya.
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…