Kitu ninachopendea Airtel ni moja tu, huduma zao za internet ni uhakika, hata kama tunalipia ni uhakika speed ipo tofauti na wale wezi niliowakimbia mwaka jana(Vodacom), tatizo la Airtel ninalolionna ni moja tu, customer care call service.
Customer care service, hivi inakuwaje huduma hii niilipie, eti nakatwa Tsh 60 ili kuongea na mtu wa huduma kwa wateja, but worse ni kwamba fedha hii inakatwa kabla ya kupewa huduma. Mara zote zaidi ya mara nane(8) nilizowahi kupiga kuongea na mtoa huduma wa wateja "VIP" sikuweza kufanikiwa, hili si sawa. Tafadhali liangalieni upya!