Airtel mmeamua kutusaliti?

Airtel mmeamua kutusaliti?

PRISCUS JR

JF-Expert Member
Joined
Oct 3, 2011
Posts
448
Reaction score
236
Nimekuwa mtumiaji mzuri wa vifurushi vya airtel na nimewashawishi ndugu rafiki wengi kuhamia mtandao huu kutokana na huduma nzuri ila leo nimeumia sana naamka asubuhi kujiunga na na kifurushi cha sh 5999 ambacho ni wiki nzima yenye dakika 200 sms nyingi tu sikumbuki kwakuwa si mpenzi wa sms, 2gb za internet ndicho kivutio kabisa.
Nimeshangaa eti wamebadiri tena bila taarifa dakika 135 , sms 1000 hazina maana kibaya zaidi net ni 500mb! hivi kweli mmeaza tabia za washindani wenu ambao nao baada ya kuanza kupoteza wateja wamejirekebisha!
Nawaambia kama niliwajenga hata kuwabomoa naweza, kuna mtandao mpaka leo wananiomba walau niweke mia nimegoma na line iko hewani tu
Mjirekebishe la sivyo tutaharibiana kaeni mfikirie upya efu sita ni pesa nyingi sana acheni utani.
 
Si wewe pekee ndugu hata mm washaanza kuniboa!Kifurushi cha 499 nilikuwa napewa dak 20 wakapunguza hadi dak 15 sasa dak 13."Tumehamia Airtel" haina maana hatuwezi "Kuhama Airtel" mkizidi zaidi tutahama maana sio ishu sana.
 
Mkuu Peter jaluo nimekusoma tigo bado wanatumikia adhabu niliyowapa kwa makosa walionifanyia nimewaharibia kweli japo hawajui moja kwa moja kama ni mimi nimewaangamiza. Tupate pesa kwa shida bado nao watuangaishe
 
Hivi TCCRA wanafanyaga kazi gani? Kama wanashindwa kutulinda dhidi ya wezi kama hawa.
 
Mkuu Peter jaluo nimekusoma tigo bado wanatumikia adhabu niliyowapa kwa makosa walionifanyia nimewaharibia kweli japo hawajui moja kwa moja kama ni mimi nimewaangamiza. Tupate pesa kwa shida bado nao watuangaishe

ehee uliwapa athabu gani mkuu, wasije wakakutafuta
 
Kwa wale kama mimi niliyokuwa na tumia bundle ya 5999 kwa wiki, na airtel kutubadilishia hizi tarriff zao wanavyotaka, nimeamua kubadilisha recharging kwa kuchagua ya 650/day. Napata dk 20, MB 150 na SMS za kimavi 450 ambazo sijui kwa nani anayehitaji sms siku hizi. Najua hii ni kazi zaidi na kudownload inakuwa limited kwa hizo 150 MB kwa siku. Lakini ni gharama nafuu kwa mwezi ukilinganisha na ile 5999 ambayo sasa hivi unapata MB 750 kwa wiki v/s MB 1050 per wk kama ukichagua 150 MB kwa siku.. dk 20 zinajumlishwa vile vile kwa dk ambazo hazikutumiwa.. kwa kifupi. Hawa Airtrl wameni punguzia gharama kati ya shilingi 3846 mpaka 4496
 
Mi karibia narudi kwenye mambo ya p.o.box .....Dar es Salaam.
Yahusu:USHOGA WETU KUYUMBA YUMBA
Husika na kichwa chs habari hapo juu .......blah blah blah.
 
Mkuu vitu_vya_watu umeniambia kitu cha maana, je usiponaliza Mb zako wanazijumulisha kesho yake? Maana walikuwa hawamfanyi hivyo?
Ujue kwa smart phone wakikupa mb kidogo wanakuwa wanakuumiza kwakuwa wengine tumeachana na Modem tunatumia simu kufanya kila kitu kinachohusu mtandao.
Ama ndio tuseme wamevuna wateja wa kutosha sasasa wanatuhujumu!
Mi nawapa angalizo, binadamu hasa mtz unapomuwekea mazingira magumu kupata kitu akipendacho unamtengenezea mazingira ya yeye kukuibia jambo ambalo ni hasara wawaulize D*TV wanavyohujumiwa na receiver ambazo zinafungua chane mpaka ambazo wao d*tv hazimo kwenye receiver zao.
Watu wa marketing mlifanyie kazi niwambie mlikuwa mmewapiga vibaya washindani wenu mpaka wameangaika kufanya marekebisho.
Naamini hakuna hasara mnayoipata kwakuwa kuna wengine hawatumii net kabisa wao ni kuongea tu na mwisho wa wiki data inabaki vile vile.
Narudia mjirekebishe mapema huku mtaani maisha si mazuri.
 
Priscus JR hio data wameamua kui-bana. Kama hujamaliza wana kwangua yoote. Mimi natumia smartphone kwa hio dawa yao ni hii.. naweka sh 650 tuu kabla sijawasha mobile data. Napata hizo 150MB zao. Kesho yake kabla ya hayo masaa 25 yao waliotoa, nacheki balance kujua data imebakia ngapi. Kwa mfano leo asubuhi nilibakia na 1.1MB. Basi nika tether na laptop kumalizia download zangu ambazo zilikuwa Pending. Hio 1.1 ilivyoisha nikazima mobile data, nikazima tethering. Nika recharge halafu nika washa tena Mobile data.. najua ni kazi kidogo lakini afadhali.
 
Jana ilinichanganya kidogo nimeunga bk 2 gafla naona dk 40 badala ya dk 60 airtel mmeanza kufulia.
 
kweli hawa watu hawana huruma ila wacpo jirekebisha haraka naangalia maslai kwingine!!!
 
Acheni kulia lia jamani nyie mnafhani gharama za uendeshaji zimepanda wao watabaki na bei hiyohiyo tu
 
Back
Top Bottom