Airtel acheni wizi

nessonlegend

JF-Expert Member
Mar 1, 2013
1,698
1,507
Mnamo tarehe 16-1-2019 nimekopa salio kupitia huduma ya airtel inayopatikana kupitia menyu *149*99# >1 ofa maalumu >3 kopa bando >4 kopa salio. katika kipengele cha namba 3 hapo kuna option za kuchagua mfano unataka kukopa muda wa hewani toka airtel kwenda airtel, au kwenda mitandao yote, au unataka kukopa kifurushi cha intaneti, pia kuna hiyo namba 4 ambayo ukiichagua ndiyo kuna option ya kiasi cha muda wa maongezi unaotaka kupatiwa.

Lakini kitu cha kushangaza ni kwamba pamoja na kuchagua muda wa hewani, wanakuletea ujumbe kuwa umepokea kiasi fulani toka huduma ya DAKA, na wakati huo huo ukiangalia salio kupitia *102# wanakuletea ujumbe kuwa hauna salio ila una deni la kiasi fulani likiwa limeongezwa na tozo kama riba ya mkopo.

Baada ya kutafakari nikapiga namba 102 ili kuangalia salio kwa njia ya sauti ndiyo wanaleta ujumbe kuwa una dakika kadhaa na deni la shilingi kadhaa. Nilikasirika sana tena sio kidogo (nilitumia hii huduma kwasababu ilikuwa usiku na nilikuwa nahitaji salio niunge night park ya GB). nikajikuta najiuliza maswali haya yafuatayo:

a) Ni kwanini wananipangia matumizi ilihali pesa wamenikopea na wanahitaji kulipwa na riba?

b) Wana uhakika gani kuwa nilikuwa nahitaji dakika za kuwasiliana na watu na wakati nimekopa muda wa maongezi?

c) Mbona kuna option yakukopa vifurushi na muda wa hewani tofauti afu mtu ukikopa muda wa hewani unapatiwa dakika bila ya maelezo yoyote?

d) Je, huu sio wizi tuaofanyiwa na huu mtandao?

e) TCRA wanajua hii dhuruma tunayofanyiwa watu tunaotomia mtandao huu?

Leo tarehe 17-1-2019 asubuhi nimelipa deni lao lakini hawaleti hata taarifa kuwa umefanikiwa kurejesha deni lako kama ilivyo katika mitandao mingine, hata dakika zao wanazoziseha sijazitumia kwani sikuwa nashida nazo. HUU WIZI TUSIFUMBIE MACHO WADAU WA JF.
 

Attachments

  • Screenshot_2019-01-16-21-40-42.png
    Screenshot_2019-01-16-21-40-42.png
    7.8 KB · Views: 27
  • Screenshot_2019-01-16-21-41-42.png
    Screenshot_2019-01-16-21-41-42.png
    12.3 KB · Views: 42
  • Screenshot_2019-01-17-09-21-33.png
    Screenshot_2019-01-17-09-21-33.png
    13.7 KB · Views: 46
  • Screenshot_2019-01-17-09-21-53.png
    Screenshot_2019-01-17-09-21-53.png
    16.7 KB · Views: 42
Ni malalamiko. Ila nawashauri wakulipe maana umewapigia promo kubwa sana.
Binafsi sikujua kama naweza kopa, Leo nitakopa
 
Watoa huduma wako wengi mkuu kama hutaki kupangiwa matumizi ya salio ulilokopa hamia vodacom wao hawatakupangia ila utajuta kwenye makato ya miamala ya pesa n.k
.
Utawakumbuka Airtel
 
Ni kama voda,ukitumiwa msg salio lako ni chini ya mb 250 then baada ya dakika 2,salio lako la mb ni 0.
 
binafsi sinaga utani hivi nimewafuata kwenye page yao FB bahati mbaya ni kwamba inakataa kupost comment kama hii maana nilitaka niwafuate hukohuko. ili kila mtu aone jinsi tunayoibiwa na hawa jamaa
 
Ungenunua muda wa maongezi kwenye akiba yako hii mikopo ya mitandao unaweza kuulipa mwaka mzima bila kujua
mkuu nilikopa ili niunge kifurushi cha usiku nilishindwa kutoka na uvivu kwenda dukani nikaona nikope asubuhi niwalipe kwa kuweka vocha tu sasa badala yake wamenigeuza msukule :mad::mad::mad::mad:
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom