Mstahiki Mea
JF-Expert Member
- Jul 13, 2018
- 5,581
- 10,110
Jinsi Rostam Aziz Alivyoingiza Zaidi ya TSh Bilioni 7 Ndani ya Siku Mbili Kupitia Hisa Bila Kuuza chochote
Kama humjui Rostam Aziz, ni mmoja wa wafanyabiashara wakubwa na wawekezaji wenye ushawishi Afrika Mashariki.
Amewekeza katika sekta nyingi kama nishati, mawasiliano na viwanda.
hiyo Siyo mada ya Leo...
wiki hii kulikuwa na jambo la kuvutia zaidi.
Rostam Aziz Kupitia kampuni yake Taarifa Ltd, Rostam Aziz alitangaza kununua 54.08% ya hisa za Nation Media Group (NMG) ya Kenya.
NMG ni moja ya makampuni makubwa ya media Afrika Mashariki inayomiliki vyombo kama:
Daily Nation
NTV Kenya
The East African
Na Tanzania wanamiliki magazeti kama:
Mwananchi
The Citizen
Mwanaspoti
Baada ya tangazo hilo…
Bei ya hisa za NMG ilipanda kwa zaidi ya 28.3% ndani ya siku mbili tu.
Kabla ya tangazo:
Hisa zilikuwa KSh 13.25
Baada ya tangazo:
Zilipanda hadi KSh 17 kwa hisa
Kwa kuwa NMG ina zaidi ya hisa milioni 190, na Rostam anamiliki zaidi ya 50%.
kupanda huko kwa bei ya hisa kuliongeza thamani ya uwekezaji wake kwa makadirio ya zaidi ya TSh bilioni 7 ndani ya siku mbili.
Na hapa ndipo siri ya uwekezaji ilipo.
Rostam hakuchapisha magazeti.
Hakuuza habari.
Hakutangaza matangazo.
Alinunua hisa.
Na thamani ya uwekezaji wake ikaongezeka kutokana na kupanda kwa bei ya hisa.
Ndiyo maana utajiri mkubwa duniani haujengwi kwa kufanya kazi tu…
Unajengwa kwa kumiliki assets kama:
Hisa za makampuni
Biashara
Uwekezaji
Kwa sababu kampuni inapokua, thamani ya hisa inapanda na wewe kama mwanahisa utajiri wako unaongezeka.
Hapa Tanzania pia kuna Dar es Salaam Stock Exchange (DSE) ambapo unaweza kununua hisa za makampuni kama:
CRDB
NMB
TBL
TCC
Vodacom
Credit: Kutoka kwa Mdau