Mambo hayaendi namna hiyo
The Boss , nakubaliana na wewe kabisa kwamba Kuna watu Wana ushabiki usio na tija hapa JF.
Nnachopinga ni kwamba, kama Leo
The Monk kaongea kuhusu jambo na kutoa maoni yake haimaanishi hawezi kutoa maoni ya kitu kingine Kwa mtizamo tofauti, inabaki kuwa hayo ni mawazo na maoni yake.
Tatizo linakuja hapa, mtu anataka kumfanya binadamu kama rejea ya kipimo na Yuko sahihi siku zote, hakuna binadamu wa aina hiyo na ni hatari sana kuweka tumaini au Imani Kwa binadamu badala ya hoja zake.
Unakuta mtu anasema namkubali sana flani, hiyo ni tatizo, yeye ana misimamo yake, maslahi yake binafsi na mitazamo tofauti kuhusu Kila jambo, lazima atabadilika kulingana na Hilo jambo linalojadiliwa.
Tusiweke nguvu kubwa sana kuunga mkono au kushabikia watu, tujikite kwenye hoja, hapo ndio itakua tumepunguza hizi sarakasi zinaziendelea.