Anicet mchomvu
Member
- Apr 18, 2012
- 95
- 213


Kuna watu wameumizwa na marafiki zao kwa sababu hawakuwa na macho ya rohoni kuweza kuwatazama.
Kama wewe ni mmoja kati ya wale ambao marafiki wamekuwa jaribu, basi somo hili na likawe msaada kwako.

Hili ni kundi la kwanza la marafiki.
“Confidants” ni wale marafiki wanaokupenda bila masharti. Wako nawe ukiwa juu au chini, ukiwa tajiri au maskini, ukiwa sahihi au ukikosea, wako pamoja na wewe. Ukipelekwa gerezani watakufuata, ukilia watalia pamoja nawe, na ukifurahi watafurahi pamoja nawe. Ni watu ambao unakuwa huru zaidi kuwaeleza kila jambo kuhusu maisha yako (kuliko hata ndugu zako) na kwa kufanya hivyo unajikuta unafarijika na kupata amani moyoni. Hutaweza kutimiza maono yako bila kuwapata “Confidants” wako.


Hawa ni marafiki hatari, kwa sababu hawako kwa ajili yako, wapo kuiba maono yako. Ni wezi wa maono. Biblia inasema pasipo maono watu huangamia (Mithali 29:18); Kwa hiyo anayekuibia maono kwa lugha nyingine amekuangamiza. Unakuta binti amepata mchumba, (au hata wakaka sometimes!!!!) anamshirikisha rafiki yake kile Bwana alichomtendea, lakini baada ya muda mfupi anaachwa na anashangaa rafiki yake mtu aliyemuamini saaaaaana amemuibia mchumba. Watu wengi wameumizwa na marafiki kwa namna hii but kiukweli hawasemi tu.. Huyo alikuwa rafiki aina ya “constituent”, unachotaka ndicho anachotaka. Ole wako wewe mwenye constituent kwenye mahusiano au biashara yako ukidhani ni confidant. Ukimueleza constituent habari za mchumba wako atakuibia (abiria chunga mzigo wako!!!) Ukimueleza constituent habari za wazo la biashara unayotaka kuanzisha atakuibia hilo wazo.


Hawa ni marafiki ambao Mungu anawaleta katika maisha yako kwa kusudi maalumu, sometimes kwa muda maalumu tu na baada ya hapo hutawaona tena. Ni watu wanaopigana na kile unachopigana nacho, kukusaidia kushinda upinzani mkubwa na baada ya hapo hutawaona tena. Sasa usipate shida wakikuacha na kuondoka, hawa hawatadumu nawe kipindi kirefu. Hawa ni kama ngazi (ladder) ambayo inahitajika sana wakati nyumba inajengwa, lakini nyumba ikishakamilika ngazi itaondolewa ila nyumba itabaki.

❇NB.
Wako marafiki wengine hawako kwenye kundi lolote kati ya hayo niliyoyataja hapo juu.
Hao nawaita “wrong partners”. Hutaweza kufika unakokwenda usipojitenga nao mapema. Mkumbuke Yona. Watu wote kwenye meli wangeangamia kama wasingemtupa Yona baharini. He was a wrong partner (japo ni mtumishi wa Mungu). Mtupe Yona wako, ili ufike salama. Kuna huduma zimekwama, kuna makampuni yamerudi nyuma, kuna biashara zimefilisika kwa sababu wamembeba Yona bila kujua atawaletea shida safarini.. mtupe
Yona wako, Tafuta Confidants wako,..